Pata taarifa kuu

Xi na Zelensky wafanya mazungumzo kwa njia ya simu

NAIROBI – Rais wa China Xi Jinping, amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky, mazungumzo ambayo ni ya kwanza kati ya viongozi hao wawili tangu uvamizi wa Ukraine.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kutoka kushoto, na mwenzake wa China Xi Jinping, kulia.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kutoka kushoto, na mwenzake wa China Xi Jinping, kulia. © CNN
Matangazo ya kibiashara

Shirika la habari la CCTV, limeripoti kuwa kwenye mazungumzo hayo, Xi, alimwambia Zelensky kuwa msimamo wa China kuhusu mgogoro wa Ukraine, ni kuwepo kwa amani na msimamo wake ni kuchangia kuwepo kwa mazungumzo ya amani.

Naye Zelensky kwenye mtandao wake wa Twitter, amesema mazungumzo haya yalikuwa yenye manufaa, ikizingatiwa kuwa mazungumzo haya ni ya kwanza kati ya viongozi hao wawili, tangu Urusi kuivamia Ukraine, mnamo Februari, 24, 2022.

Naamini kuwa mazungumzo haya ya simu, vilevile kuteuliwa kwa balozi wa Ukraine nchini China, itatoa msukumo mkubwa katika maendeleo ya uhusiano wetu wa nchi mbili,"Ameandika Zelensky kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Pavel Ryabikin, ambaye alikuwa akiiongoza wizara ya kampuni za kimkakati ya Ukraine, ndiye balozi mpya wa Ukraine nchini China, kwa mujibu wa amri ya rais iliyochapishwa kwenye wavuti.

Ukraine haijakuwa na balozi nchini China tangu Februari mwaka 2021.

Naye msemaji wake Sergiy Nykyforov, amesema kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa wawili hao wamezungumza kwa takriban saa limoja.

Mwezi Februari, utawala wa Beijing ilizindua waraka wenye hoja 12 ya kutaka mgogoro wa Ukraine kusuluhishwa kisiasa.

Hoja ya kwanza katika waraka huo ilikuwa kwamba uhuru na uadilifu wa eneo la nchi zote lazima udumishwe ipasavyo.

Jumuiya ya kimataifa inapaswa kusalia na kujitolea kwa njia sahihi ya kukuza mazungumzo ya amani, kusaidia pande zinazohusika kufungua mlango wa suluhu la kisiasa haraka iwezekanavyo, na kuunda mazingira na majukwaa ya kuanza tena mazungumzo," Waraka huo ulisoma.

Ni waraka ambao ulikabiliwa na mashaka kutoka kwa washirika wa Ukraine, huku mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akisema Beijing haiwezi kuaminika sana kwa sababu haijaweza kulaani uvamizi haramu wa Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.