Pata taarifa kuu

Comoro/France: Mahakama yasitisha kufurushwa kwa watu kutoka kisiwa cha Mayotte

NAIROBI – Mahakama  katika kisiwa cha Mayotte kinachomilikiwa na Ufaransa, imezuia mpango wa serikali, kuwaondoa wahamiaji waliongia katika kisiwa hicho, hali iliyosababisha mvutano na kisiwa jirani cha Comoro.

Eneo la Bahari ya Hindi la Ufaransa la Mayotte liko karibu na pwani ya mashariki ya bara la Afrika.
Eneo la Bahari ya Hindi la Ufaransa la Mayotte liko karibu na pwani ya mashariki ya bara la Afrika. AP - Sony Ibrahim Chamsidine
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Ufaransa, ilikuwa imepanga kuanzisha operesheni hiyo iliyopewa jina Wuambushu au Chukua kwa lugha ya asili, kwa lengo la kuwaondoa wageni waliongia katika kisiwa hicho, kwa kile inachosema inataka kuhakikisha maisha yanakuwa mazuri kwa wakaazi wake.

Maafisa wa usalama wapatao 1,800, wakiwemo mamia kutoka Paris, walikuwa tayari katika kisiwa hicho kuanza operesheni hiyo katika Wilaya ya Tsoundzou, kabla ya Mahakama kusitisha zoezi hilo.

Mahakama katika mji wa Mamoudzou imesema zoezi  hilo la kuwaondoa wahamiaji hao, wengi kutoka Comoro katika mtaa wa mabanda wa Koungou, hauna msingi wa kisheria.

Mamlaka nchini humo imesema itakata rufaa uamuzi huo.

Uongozi wa Kisiwa cha Comoro, ulio Kaskazini Magahribi kisiwa cha Mayotte, ulikataa kuruhusu boti iliyokuwa imebeba wahamiaji kutoka kwenye kisiwa hicho cha Ufaransa inachosema ni eneo lake.

Mpango ni kwamba wale wasio na karatasi warudishwe katika kisiwa cha Comoran cha Anjouan, kilomita 70 (maili 45) kutoka Mayotte.

Mnamo mwaka wa 2019, Ufaransa iliahidi euro milioni 150 kama msaada wa maendeleo kama sehemu ya mpango wa kukabiliana na biashara haramu ya binadamu na kurahisisha urejeshwaji wa raia wa Comoro kutoka Mayotte.

Mayotte ni kisiwa cha nne cha visiwa vya Comoro ambacho Ufaransa ilishikilia baada ya kura ya maoni ya awali ya 1974, lakini bado inadaiwa na Moroni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.