Pata taarifa kuu
VITA-HAKI

Video ya mfungwa wa Ukraine aliyekatwa kichwa: UN yasema 'kuhuzunishwa', EU 'kudai haki'

Video ya mtu anayedhaniwa kuwa mfungwa wa Ukraine ambaye amekatwa kichwa hivi punde na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Urusi yazua malalamiko na huzuni duniani.

Askari wa Ukraine karibu na uwanja wa vita huko Bakhmout mashariki mwa nchi, Aprili 10, 2023.
Askari wa Ukraine karibu na uwanja wa vita huko Bakhmout mashariki mwa nchi, Aprili 10, 2023. © LIBKOS / AP
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kutetea haki za binadamu nchini Ukraine umesema "umeshtushwa" siku ya Jumatano na video iliyoonekana mtandaoni ikionyesha mwanajeshi wa Urusi akimkata kichwa mfungwa wa Ukraine kwa kisu. Pia ujumbe huo unataja video ya pili inayoonyesha "miili iliyokatwakatwa, ambayo inaonekana ni ya wafungwa wa vita wa Ukraine", na kwa hivyo unataka "matukio haya yawe yafanyiwa uchunguzi wa kweli na wahusika wawajibishwe".

Umoja wa Ulaya unasema utawawajibisha wahalifu wa kivita nchini Ukraine, kwa mujibu wa msemaji wake.

Mapema siku ya Jumatano, Aprili 12, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alishutumu "kunyongwa kwa mateka wa Ukraine", katika ujumbe uliorushwa kwenye Telegraph. "Ni video ya Urusi kama ilivyo. Kila mtu anapaswa kuchukua hatua. Kila kiongozi. Hatutasahau chochote. Kushindwa kwa ugaidi ni muhimu," alisema, akimaanisha "zimwi la mauaji" ya Urusi. Hadi sasa, video hiyo haijathibitishwa na mamlaka ya Urusi. Uchunguzi unafunguliwa nchini Ukraine na idara ya kijasusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.