Pata taarifa kuu

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuzuru Uholanzi

NAIROBI – Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, hivi leo anatarajiwa kuanza ziara yake nchini Uholanzi,ziara inayokuja baada ya kutembelea nchini China alikokutana na rais Xi.

Emmanuel Macron, Rais wa Ufaransa
Emmanuel Macron, Rais wa Ufaransa AP - Aurelien Morissard
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii inakuja wakati huu kukishuhudiwa hsia mseto juu ya matamshi yake yenye utata kuhusu uhusiano wa bara ulaya na Marekani na China aliyoyatoa wakati wa ziara yake nchini China.

Macron, ambaye juma lililopita alifanya zaira nchini China, amekabiliwa na ukosoaji mkubwa baada yake katika mahojiano yaliochapishwa jumapili kusema kuwa sio lazima kwa Ulaya kuwa mfuasi wa Marekani au China kuhusu suala la Taiwan.

Matamshi yake hata hivyo yanatishia kufunika ziara yake ya siku mbili, inayolenga kuangazia hali mpya kati ya Paris na the Hague, haswa baada ya mabadiliko ya Brexit.

Macron ambaye ameandamana na mke wake, na mawaziri saba, baadaye leo jioni, Macron anatarajiwa kutoa hotuba juu ya umoja wa bara ulaya katika masuala ya usalama na uchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.