Pata taarifa kuu

Uholanzi:Makumi ya watu wauguza majeraha baada ya ajali mbaya ya Treni

Nairobi – Mtu mmoja afariki dunia na wengine 30 kujeruhiwa vibaya baada ya treni waliokua wameabiri  kuacha njia magharibi mwa Uholanzi na kusababisha ajali jana usiku..

Treni yasababisha ajali nchini Uholanzi
Treni yasababisha ajali nchini Uholanzi 路透社
Matangazo ya kibiashara

Kulingana  na taarifa ni kuwa ajali hio ilitokea mwendo wa saa tisa usiku 03:25 am baada ya  treni iliyokuwa ikisafirisha takriban watu 60 kugonga vifaa vya ujenzi karibu na kijiji cha Voorschoten.

Kufikia sasa shughuli ya uokozi inaendeela huku madaktari na Magari kadhaa ya kubebea wagonjwa yakionekana yakiwa yamesimama tayari kuwasafirisha majeruhi.

Picha kutoka eneo la tukio zimeonyesha mabehewa yaliyopinduka, na moshi mwingi ukipanda angani .

Huduma kwenye kiungo hicho chenye shughuli nyingi zinazotumiwa na treni kutokea Amsterdam hadi Brussels na paris zimesitishwa na huenda zikarejea  tena kuanzia alasiri.

Visa kama hivi vimewai kushuhudiwa nchini humo ambapo Mwaka 2016 ajali kama hiyo  ilitokea na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine saba kujeruhiwa baada ya treni kugongana na kreni ya maji.

Mwaka 2012 mwezi Aprili mtu mwingine alifariki na wengine 117 kujeruhiwa katika mgongano karibu na Amsterdam na ripoti baadae zika sema kuwa dereva wa treni hiyo alishindwa kuheshimu ishara ya kusimama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.