Pata taarifa kuu
VITA-ULINZI

Vita nchini Ukraine: Jeshi la Urusi lajaribu kuzingira Bakhmut

Jeshi la Urusi limeongeza mashambulizi karibu na mji makao makuu ya jimbo la Bakhmout ambapo hali "ya wasiwasi" imetanda, kulingana na jeshi la Ukraine. Jeshi la Urusi, ambalo limedhibiti sehemu kubwa katika jumbo hili la mashariki linalokumbwa na mapigano, sasa linajaribu kuuzingira mji mkuu wa jimbo la Bakhmut.

Moja ya maeneo ya jimbo la Bakhmut.
Moja ya maeneo ya jimbo la Bakhmut. © REUTERS/Clodagh Kilcoyne
Matangazo ya kibiashara

Barabara tatu kati ya nne kuu zinazowezesha raia wa Ukraine kuingia mjini sasa zinadhibitiwa na vikosi vya Urusi. Barabara ya mwisho iko chini ya shinikizo kutoka kwa jeshi la Urusi ambalo linajaribu kuikaribia kutoka kusini mwa nchi.

Kulingana na kamandi ya jeshi la ardhini la Ukraine, wapiganaji wa kundi la mamluki la Wagner ndio wanaendesha mashambulizi haya, "wametuma vitengo vyao vilivyoandaliwa vyema kushambulia na wanajaribu kuvunja ulinzi wa askari wa Ukraine na kuzingira mji mkuu wa Bakhmut,” Kamanda Oleksandre Syrsky amesema Jumanne asubuhi.

Bw. Zelensky alikiri jana usiku kwamba hali karibu na Bakhmut inazidi kuwa "tata zaidi" kwa wanajeshi wa Ukraine.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilidai kuhusika na uharibifu wa ghala la silaha karibu na Bakhmout na kunasa ndege zisizo na rubani na makombora ya Himar yaliyorushwa na Waukraine. Kulingana na Taasisi ya Utafiti wa Vita "Institute for the Study of War", iliyonukuliwa na shirika la habari la AFP, Urusi "inatekeleza mbinu mpya za kushambulia" kwa kuunda vikundi vidogo na ambavyo viko katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.

Mashambulio dhidi ya Bakhmut yamekuwa yakiendelea kwa miezi sita, na katika wiki za hivi karibuni mkuu wa Wagner, Evgueni Prigojine, alitangaza kuchukuwa udhibiti wa maeneo kadhaa katika jimbo hilo: Soledar mnamo mwezi Januari, Krasna Gora mnamo mwezi Februari na hivi karibuni kuanguka kwa kijiji kidogo  cha Laguidné, kinachoungana na mji upande wa kaskazini-magharibi.

Kulingana na gavana wa jimbo la Donetsk, kulikuwa na raia 5,000, ikiwa ni pamoja na watoto 140, walioachwa huko Bakhmut katikati ya mwezi wa Februari, kati ya wakazi 70,000 kabla ya vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.