Pata taarifa kuu

Makumi ya wahamiaji wafariki baada ya boti yao kuzama karibu na pwani ya Italia

Takriban wahamiaji 59, ikiwa ni pamoja na mtoto mchanga wa miezi michache, wamefariki baada ya boti waliokuwemo kuzama, alfajiri ya Jumapili hii, Februari 26, karibu na mji wa Italia wa Crotone, huko Calabria (Kusini), kulingana na tathmini mpya ya Meya wa Crotone, Vincenzo Voce.

Waokoaji wakiokoa mwili kwenye ufuo karibu na Cutro, kusini mwa Italia, baada ya boti lililokuwa limebeba wahamiaji kuzama baharini, Jumapili, Februari 26, 2023.
Waokoaji wakiokoa mwili kwenye ufuo karibu na Cutro, kusini mwa Italia, baada ya boti lililokuwa limebeba wahamiaji kuzama baharini, Jumapili, Februari 26, 2023. © AP - Giuseppe Pipita
Matangazo ya kibiashara

Watu 70 wamenusurika katika ajali hiyo wakiwemo 21 ambao wamelazwa hospitalini. Zoezi la kutafuta miili ya watu wengine linaendelea kwa shida sana kwa sababu ya hali ya hewa, upepo mkali na mawimbi makubwa.

"Mamia na makumi ya wamekufa maji, wakiwemo watoto, wengi wametoweka. Calabria iko katika maombolezo ya msiba huu mbaya. Lakini Ulaya iko wapi? ", Roberto Occhiuto, rais wa eneo hilo amelalamika katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Boti ya takriban mita ishirini ambayo ilisafirisha takriban "wahamiaji 250" kulingana na baadhi ya shuhuda, kutoka Uturuki, anaripoti mwandishi wetu huko Roma, Anne Le Nir. Kwa mujibu wa waokoaji waliokuwa kazini tangu asubuhi ya Jumapili hii, boti iliyojaa wahamiaji wenye asili ya Afghanistan, Iran na Pakistan ilizama, kutokana na dhoruba kali, dhidi ya miamba karibu na ufuo wa Steccato di Cutro.

Boti iliondoka kwenye bandari ya Smirna siku nne zilizopita. Ndege ya Frontex iliiona karibu na Crotone jana jioni na kutoa taarifa ya uokoaji wa baharini kutoka Taranto na Crotone. Lakini hali mbaya ya hewa ilizuia kufikia eneo hilo. 

Waziri Mkuu Giorgia Meloni ameelezea katika taarifa yake "maumivu makubwa kwa waathiriwa wa wasafirishaji haramu wa binadamu na akasisitiza dhamira ya serikali yake ya kuzuia uhamiaji haramu". Waziri wa Mambo ya Ndani, Matteo Piantedosi alimuunga mkono kwa kuzungumzia "janga kubwa linalodhihirisha kuwa ni muhimu kupambana na mitandao ya wahamiaji haramu".

Kwa upande wake, shirika lisilo la kiserikali la Sea Watch liliandika kwenye Twitter "kutokuwepo kwa ujumbe wa utafiti wa Ulaya ni uhalifu unaorudiwa kila siku". 

Shuhuda zilizokusanywa na vyombo vya habari vya Italia, hasa zile kutoka kwawaokoaji, ni za kuhuzunisha. Moja inasema kwamba ni wale tu ambao waliweza kuruka kutoka kwenye bot waliweza kunusurika, wale ambao walikuwa wamerundikana katika boti wote walifariki. Picha zinaonyesha miili iliyofunikwa kwenye begi nyeupe ya plastiki yenye nambari iliyoandikwa kwenye kila mfuko.

Ajali hiyo mpya ya meli inakuja siku chache tu baada ya bunge kupitisha sheria mpya zenye utata na serikali yenye siasa kali za mrengo wa kulia juu ya kuwaokoa wahamiaji. Mkuu wa serikali Giorgia Meloni, kiongozi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Fratelli d'Italia (FDI), alichukua wadhifa wa kiongozi mkuu wa muungano mwezi Oktoba baada ya kuahidi kupunguza idadi ya wahamiaji wanaowasili Italia.

Sheria hiyo mpya inazitaka meli za kibinadamu kufanya uokoaji mmoja tu kwa wakati mmoja, jambo ambalo wakosoaji wanasema linaongeza hatari ya vifo katika eneo la kati la Mediterania ambalo kivuko chake kinachukuliwa kuwa hatari zaidi duniani kwa wahamiaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.