Pata taarifa kuu
NEW ZEALAND- SIASA

New Zealand: Waziri mkuu Jacinda Ardern kujiuzulu mwezi ujao

Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern, ametangaza kuwa atajiuzulu mwezi ujao, kufuatia kile anachosema hana nguvu za kuendelea kuwa kiongozi wa nchi hiyo. 

Jacinda Ardern, Waziri Mkuu wa  New Zealand
Jacinda Ardern, Waziri Mkuu wa New Zealand AP - Seth Wenig
Matangazo ya kibiashara

“Natangaza sitawania tena nafasi ya uwaziri mkuu na nitaondoka katika ofisi kama waziri mkuu mwezi Februari.”

Tangazo lake linakuja baada ya chama chake cha Labour kuonekana kuanza kupoteza umaarufu.  

Ardern, ambaye amekuwa madarakani kwa karibu miaka sita, atakumbukwa kwa namna alivyoongoza nchi yake kukabiliana na maambukizi vya Uviko 19, nchi yake ikiandikisha  idadi ndogo ya maambukizi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.