Pata taarifa kuu

Mateka wa Ujerumani aliyeshikiliwa katika Sahel kwa zaidi ya miaka minne hatimaye aachiliwa

Jörg Lange, Mjerumani mwenye umri wa miaka 63 ambaye ni mhudumu wa kibinadamu, alishikiliwa kama mateka huko Sahel kwa zaidi ya miaka minne. Kuachiliwa kwake kuliwezekana kupitia Morocco, kulingana na vyombo vya habari vya Ujerumani.

Jörg Lange alitekwa nyara mnamo Aprili 11, 2018 magharibi mwa Niger na watu wenye silaha waliokuwa na pikipiki karibu na eneo la Ayorou.
Jörg Lange alitekwa nyara mnamo Aprili 11, 2018 magharibi mwa Niger na watu wenye silaha waliokuwa na pikipiki karibu na eneo la Ayorou. AP - Rebecca Blackwell
Matangazo ya kibiashara

Jörg Langer alirudishwa nyumbani kwa ndege ya jeshi. Kulingana na gazeti la Der Spiegel, mhudumu huyo wa kibinadamu mwenye umri wa miaka 63 “anaendelea vyema, kutokana na hali ilivyo. "Tunawashukuru kwa moyo mkunjufu watu wote ambao wamechangia kuachiliwa huku au ambao wameunga mkono, hasa kitengo cha shida cha Wizara ya Mambo ya Nje, polisi wa uhalifu na mamlaka na marafiki huko Mali, Niger na katika nchi jirani". alitoa maoni kwa shirika la misaada ya kibinadamu ambapo anafanyia kazi.

Vyombo vya habari vya Ujerumani vinahakikisha kwamba Morocco ilichukua jukumu muhimu katika mazungumzo na watekaji nyara.

Takriban mateka wanne wa nchi za Magharibi bado wanazuiliwa katika uknda wa Sahel, akiwemo Mfaransa Olivier Dubois. Na tangu mwisho wa mwezi wa Novemba, hazijapatikana habari za kasisi wa Kikatoliki wkutoka Ujerumani Hans Joachim Lohre, pengine alitekwa nyara huko Bamako.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.