Pata taarifa kuu

Kremlin: Vladimir Putin atazuru Donbass 'kwa wakati ufaao'

Rais wa Urusi bado hajatembelea eneo hili la mashariki mwa Ukraine, ambalo alilinyakua mwishoni mwa mwezi Septemba, bila hata hivyo jeshi lake kudhibiti kikamilifu. "Kwa wakati ufaao, bila shaka, (ziara kama hiyo) itafanyika. Ni eneo la Urusi,” msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov amewaambia wanahabari alipoulizwa kuhusu uwezekano wa ziara ya Bw. Putin huko Donbass katika siku za usoni.

Kulingana na watu kadhaa au vyombo vya habari, Putin kwa sasa ametengwa sana huko Kremlin, anahisi kutishiwa kisiasa na hata kimwili.
Kulingana na watu kadhaa au vyombo vya habari, Putin kwa sasa ametengwa sana huko Kremlin, anahisi kutishiwa kisiasa na hata kimwili. © AP/Mikhail Metzel
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya Kremlin imetangaza kuwa rais wa Urusi atazuru eneo hili la mashariki mwa Ukraine, lililonyakuliwa mwezi Septemba lakini kwa kiasi fulani likidhibitiwa na Kyiv, bila kutaja tarehe.

Vladimir Putin atakwenda Donbass "kwa wakati ufaao", Kremlin imesema Jumamosi, wakati rais wa Urusi bado hajatembelea eneo hili la mashariki mwa Ukraine ambalo alilinyakua mwishoni mwa mwezi Septemba, bila hata hivyo, jeshi lake kudhibiti kikamilifu.

"Kwa wakati ufaao, bila shaka, (ziara kama hiyo) itafanyika. Ni eneo la Urusi,” msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari alipoulizwa kuhusu uwezekano wa Putin kuhamia Donbass katika siku za usoni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.