Pata taarifa kuu

Maporomoko ya ardhi nchini Italia: Idadi ya vifo yaongezeka hadi watu wanane

Maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa katika kisiwa kidogo cha Ischia nchini Italia siku ya Jumamosi yaliua watu wanane, kulingana na ripoti mpya iliyochapishwa na mamlaka siku ya Jumatatu.

Watu wakiondoa tope baada ya mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha maporomoko ya ardhi ambayo yaliporomosha majengo na takriban watu 12 hawajulikani waliko, huko Casamicciola, kisiwa cha Ischia kusini mwa Italia, Jumapili, Novemba 27, 2022.
Watu wakiondoa tope baada ya mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha maporomoko ya ardhi ambayo yaliporomosha majengo na takriban watu 12 hawajulikani waliko, huko Casamicciola, kisiwa cha Ischia kusini mwa Italia, Jumapili, Novemba 27, 2022. AP - Salvatore Laporta
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya hapo awali iliripoti watu 7 waliofariki dunia. Watu wanne pia bado hawajulikani walipo, kulingana na ripoti ya hivi punde iliyotolewa siku ya Jumatatu na wilaya ya Naples (kusini) ambayo inaungana na Casamicciola Terme, kituo cha mapumziko cha wakaazi 8,000 kwenye kisiwa hiki kilicho katika Ghuba ya Naples.

Serikali imetangaza hali ya hatari kwa Ischia, hali ambayo inatoa utaratibu wa kuharakishwa kwa kukusanya fedha na rasilimali, ikiwa ni pamoja na zile za ulinzi wa raia, kwa uingiliaji kati wa haraka au kuanzishwa kwa miundo ya mapokezi.

Zaidi ya waokoaji 650 wametumwa kisiwani humo kushiriki shughuli za utafutaji na uokoaji manusura wa janga hili ambalo pia limesababisha watu watano kujeruhiwa na wakazi 230 wa kisiwa hicho kukosa makazi baada ya kuharibu nyumba thelathini.

Maafa hayo yalisababishwa na kuunganishwa kwa mambo kadhaa: ukataji miti, maendeleo makubwa ya mali isiyohamishika, pamoja na ukosefu wa usafi na kukinga.

Kulingana na mwanajiolojia aliyenukuliwa Jumatatu na gazeti la kila siku la Il Corriere della Sera, hali bado ni hatari: "sehemu nzuri ya mteremko wa kaskazini wa kisiwa hicho na hasa Casamicciola terme, baada ya maporomoko ya siku mbili zilizopita, bado iko hatarini", ameonya Aniello Di Iorio baada ya ukaguzi kwenye eneo la tukio.

Gazeti la kila siku la Il Corriere della Sera pia linamnukuu meya wa zamani wa Casamicciola, Giuseppe Conte, ambaye anadai kuwa alitahadharisha tawala kadhaa juu ya hatari ya maporomoko ya ardhi siku nne kabla ya janga hilo. "Nilikuwa nimemwandikia gavana wa Naples, kwa ulinzi wa raia wa Naples (...) Hakuna aliyenijibu", amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.