Pata taarifa kuu
UHURU-KISIASA

Mahakama ya Juu ya Uingereza haitaki kura nyingine ya maoni kuhusu uhuru wa Scotland

Hakutakuwa na kura mpya ya maoni kuhusu uhuru wa Scotland. Mahakama ya Juu ya Uingereza imetoa uamuzi huo Jumatano, Novemba 23, baada ya majuma kadhaa ya mashauriano. Waziri Mkuu wa Scotland, Nicola Sturgeon ndiye aliyewasilisha malalamiko yake kuhusiana na uhuru wa Scotland. Majaji wanaona kuwa Scotland haina uhalali wa kuandaa kura hiyo.

Nicola Sturgeon, hapa ilikuwa Jumatatu, Novemba 21, 2022.
Nicola Sturgeon, hapa ilikuwa Jumatatu, Novemba 21, 2022. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Bunge la Scotland haliwezi kushauriana na raia wake kuhusu uhuru wa taifa hilo bila idhini ya Bunge la Kitaifa la Uingereza huko Westminster, Mahakama ya Juu imebaini... Ridhaa ambayo Wabunge wa pande zote wa Westminster wanakataa kutoa - kwa wakisema wakazi wa Scotland tayari wamepiga kura , miaka minane iliyopita, kuendelea kuungana na Uingereza kama taifa moja, na Brexit haitoshi kuhalalisha kura ya pili ya maoni.

Kesi ya kikatiba

Katika hukumu yake ya kurasa 35, Mahakama ilizingatia mswada wa sheria wa Edinburgh. Ingawa matokeo ya kura ya maoni hayatakuwa ya lazima kisheria, yatakuwa na athari za kisiasa kiasi kwamba ni suala la kikatiba. Na kwa hiyo, inahusu moja kwa moja London.

Maandamano ya Kitaifa

Iwapo Nicola Sturgeon aliomba maoni ya Mahakama ya Juu, ilikuwa ni kuhakikisha kwamba kura hiyo ya maoni isingepingwa. Kwa hivyo pengine hakutakuwa na kura mnamo mwezi Oktoba 2023, kama alivyotaka Waziri Mkuu - lakini tayari ameashiria kwamba atafanya kampeni, wakati wa uchaguzi ujao wa wabunge mnamo 2024, kuhusu suala la uhuru. Maandamano yamepangwa kote Scotland Jumatano hii, Novemba 23.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.