Pata taarifa kuu
SCOTTLAND-LIBYA-HAKI

Mahakama Kuu ya Scottland kutoa uamuzi kuhusu shambulizi la Lockerbie

Mahakama Kuu ya Scottland inatarajia kutoa uamuzi wake leo Jumanne kuhusu rufaa dhidi ya hukumu kwa raia mmoja wa Libya aliyehukumiwa kwa kuandaa mashambulizi ya mwaka 1988 dhidi ya ndege ya Pan Am ambayo ililipuka juu ya anga ya Scottland, na kuua watu 270.

Ndege ya Pan Am Boeing 747, ambayo ilikuwa ikifanya safari ya London kwenda New York, ililipuka juu ya anga ya mji wa Scotland wa Lockerbie Desemba 21, 1988, na raia wengi wa Marekani walikuemo wakirudi Marekani kwa sikukuu za mwisho wa mwaka.
Ndege ya Pan Am Boeing 747, ambayo ilikuwa ikifanya safari ya London kwenda New York, ililipuka juu ya anga ya mji wa Scotland wa Lockerbie Desemba 21, 1988, na raia wengi wa Marekani walikuemo wakirudi Marekani kwa sikukuu za mwisho wa mwaka. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hili lilikuwa shambulio baya zaidi la kigaidi katika historia ya Uingereza. Ndege ya Pan Am Boeing 747, ambayo ilikuwa ikifanya safari ya London kwenda New York, ililipuka juu ya anga ya mji wa Scotland wa Lockerbie Desemba 21, 1988, na raia wengi wa Marekani walikuemo wakirudi Marekani kwa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Mnamo 2001, afisa wa ujasusi wa Libya Abdel Basset al Megrahi alihukumiwa kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kuua abiria 243, wafanyakazi 16 na wakaazi 11 wa mji wa Lockerbie waliouawa katika shambulio hilo.

Megrahi, ambaye kila wakati alidai kuwa hana hatia, alifariki dunia nchini Libya mnamo mwaka 2012, miaka mitatu baada ya kuachiliwa huru na serikali ya Scottland kwa sababu za kibinadamu baada ya kugundulika na ugonjwa sugu wa saratani.

Mnamo mwezi Machi mwaka huu, shirika huru liliamua kwamba familia ya Megrahi ilikuwa na haki ya kukata rufaa baada ya kuona kwamba kulikuwa na makosa ya kisheria. Mpaka sasa Megrahi ndiye pekee aliyehukumiwa katika kesi hii.

Rufaa ya kwanza iliyowasilishwa mahakamani mwaka 2002 ilikataliwa na Mahakama Kuu. Rufaa nyingine ilifutiliwa mbali mnamo mwaka 2009 kabla tu ya Megrahi kurudi Libya.

Mnamo mwaka 2003, kiongozi wa Libya wa wakati huo Muammar Gadhafi alitambua kwamba nchi yake ilihusika katika shambulio hilo na kufidia familia za wahanga, bila hata hivyo kukiri kwamba alitoa agizo la kutekelezwa kwa shambulio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.