Pata taarifa kuu
UINGEREZA-SCOTLAND-UHURU

Scotland kutaka kuwa uhuru kupitia kura ya maoni

Kiongozi wa serikali ya Scotland Nicola Sturgeon, ametangaza kwamba ataomba ruhusa ya kufanywa kura ya maoni ya pili kuhusu uhuru wa jimbo la Scotland.

Nicola Sturgeonkiongozi wa serikali ya Scotland
Nicola Sturgeonkiongozi wa serikali ya Scotland EUTERS/Russell Cheyne
Matangazo ya kibiashara

Nicola Sturgeon amebaini kwamba hatua hiyo inahitajika ili kulinda maslahi ya Scotland baada ya Uingereza kupiga kura ya kuondoka katika Umoja wa Ulaya.

Bi Sturgeon amesema kuwa anataka kura kufanyika kati ya mwaka 2018 na 2019, huku akisema kuwa ataliomba bunge la Scotland wiki ijayo kuomba amri kutoka kwa bunge la Uingereza.

Waziri mkuu Theresa May hajatamka lolote ikiwa ataruhusu kura hiyo ifanyike wala kutoa nafasi jimbo hilo liwe huru na kutotegemea serikali ya Ungereza.

Msemaji Theresa May amesema kuwa ushahidi ulionyesha wazi kuwa watu wengi hawataki kura ya maoni ya pili ifanyike.

Wadadisi wanasem aikiwa serikali ya Uingereza itaruhusu kura hiyo ipigwe kuna hatari majimbo mengine yanayounga Uingereza kuomba ruhusa kuhusu uhuru wa majimbo yao. Lakini wamesema kuwa hawana imani kuwa serikali ya Uingereza itaruhusu kura hiyo ifanyike.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.