Pata taarifa kuu

Ufaransa: Watu ambao waliokuwa katika meli ya 'Ocean Viking' wawekwa katika eneo la kusubiri

Meli iliyobeba wahamiaji 230 imetia nanga katika bandari ya Toulon nchini Ufaransa, baada ya kuzuka kwa mvutano kati ya nchi hiyo na Italia kuhusu ni taifa lipi linapaswa kuwapokea.

Watu walioshuka kutoka meli 'Ocean Viking' watahamishiwa kwenye rasi ya Giens huko Hyères. Zaidi ya watoto hamsini walikuwemo, Novemba 11, 2022.
Watu walioshuka kutoka meli 'Ocean Viking' watahamishiwa kwenye rasi ya Giens huko Hyères. Zaidi ya watoto hamsini walikuwemo, Novemba 11, 2022. AP - Vincenzo Circosta
Matangazo ya kibiashara

Meli hiyo, Ocean Viking, inayomilikiwa na Shirika lisilo la kiserikali la Ufaransa, liliwaokoa wahamiaji hao Pwani ya Libya, na imekuwa ikitafuta nchi ya kuwakubali wahamiaji hao. 

Ufaransa haijawaji kuwakubali wahamiaji waliookolewa kutoka Bahari ya Meditterian lakini ililazimika kuwakubali hawa  baada ya kukataliwa na nchi ya Italia. 

Siku ya Alhamisi, Waziri wa Mambo ya ndani wa Ufaransa Gerald Darmanin, alisema lilikuwa jukumu la Italia kuwapokea wahamiaji hao kwa mujibuwa sjeria za Umoja wa Ulaya, lakini nchi yake imewakubali kwa sababu za kibinadamu . 

Awali, meli hiyo ilipaswa kufikia nchini Italia kwa sababu ilikuwa karibu na êneo ambalo wahamiaji hao waliokolewa na ripoti zinasema afya zao za afya hazikuwa nzuri. 

Ufaransa imeishutumu Italia kwa kukosa ubinadamu kwa kuwakataa wahamiaji hao, kitendo ambacho kimeikarisha nchi hiyo na Waziri wake Mkuu Giorgia Meloni. 

Kitendo hiki kinaelezwa huenda kikaharibu uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.