Pata taarifa kuu
Ufaransa - siasa

Ufaransa: Rais wa Ufaransa afanyia baraza la mawaziri mabadiliko

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amelifanyia baraza lake la mawaziri mabadiliko, baada ya chama chake kupoteza idadi kubwa ya wabunge kwenye uchaguzi wa mwezi uliopita.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu Élisabeth Borne, kwa kumbukumbu ya miaka 82 ya rufaa ya Juni 18, kwenye ukumbusho wa Mont Valérien huko Suresnes karibu na Paris, Juni 18, 2022
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu Élisabeth Borne, kwa kumbukumbu ya miaka 82 ya rufaa ya Juni 18, kwenye ukumbusho wa Mont Valérien huko Suresnes karibu na Paris, Juni 18, 2022 AFP - GONZALO FUENTES
Matangazo ya kibiashara

Katika mabadiliko hayo ya bazara la mawaziri, Macron amemuacha nje waziri wa utangamano, Damien Abad,  ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ukabaji.

Hata hivyo rais  Macron, hajafanyia mabadiliko wizara muhimu kama ile ya fedha imesalia na waziri Bruno Le Maire, mambo ya nje Catherine Colonna, elimu Eric Dupond-Moretti,  ulinzi Sébastien Lecornu na wizara ya mambo ya ndani kusalia pia na Gerald Darmanin, ambaye pia anakabiliwa na tuhuma za ubakaji na hivi karibu kutuhumiwa vurugu   zilizoshuhudiwa katika uga wa Saint Denis wakati wa fainali ya mechi ya mabingwa wa ligi barani ualaya.

Katika hatua nyingine shirika la kiraia la Greenpeace, limekosoa uteuzi wa Christophe Béchu, kuwa waziri wa mazingira, likisema hana tajiriba ya maswala ya mazingira kuongoza wizara hiyo.

Kupitia taarifa shirika hilo pia limelalamikia ukosefu wa wizara ya mazingira kukosa udhabiti baada  kuwa na wamawaziri sita kwa kipindi cha miaka tano iliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.