Pata taarifa kuu

Mkutano wa Davos: Zelensky atoa wito wa vikwazo vya "kiwango cha juu" dhidi ya Urusi

Katika siku ya 89 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumatatu hii, Mei 23, fuata moja kwa moja habari za hivi punde kuhusu mzozo huo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akihutubia hadhira iliyokusanyika kutoka Kyiv wakati wa Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos, Uswidi, Jumatatu, Mei 23, 2022.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akihutubia hadhira iliyokusanyika kutoka Kyiv wakati wa Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos, Uswidi, Jumatatu, Mei 23, 2022. AP - Markus Schreiber
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Vikwazo vya jumuiya ya kimataifa dhidi ya Moscow "vinapaswa kuwa vya juu zaidi", ikiwa ni pamoja na "kutofanya biashara na Urusi", ametangaza rais wa Ukraine wakati akihutubia katika mkutano kwa njia ya video wakati wa mkutano wa Jukwaa la Uchumi la Dunia huko Davos.

► Mwanajeshi wa kwanza wa Urusi aliyehukumiwa kwa uhalifu wa kivita tangu Urusi ilipoivamia Ukraine alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela Jumatatu hii huko Kyiv.

► Sheria ya kijeshi na uhamasishaji wa jumla nchini Ukraine umeongezwa kwa miezi mitatu, hadi Agosti 23.

► Mapigano yanapamba moto huko Donbass, mashariki mwa Ukraine, huku Waziri wa Ulinzi wa Urusi akisema kuwa ushindi wa eneo la Luhansk unakaribia kukamilika. Katika eneo hili, Sievierodonetsk na Lyssytchansk, ambazo sasa zimezingirwa na vikosi vya Urusi, ni ngome ya mwisho ya upinzani wa Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.