Pata taarifa kuu
Sri Lanka

Mji wa Colombo washuhudia utulivu baada ya kutangazwa kwa hali ya dharura.

Hali ya utulivu mapema leo imeonekana kurejea katika mji wa kibiashara wa Colombo nchini Sri Lanka, Utulivu unaoshuhudiwa baada ya agizo la rais Gotabaya Rajapaksa, kutangaza hali ya dharura kufuatia ongezeko la maandamano dhidi ya serikali yake.

Walinda usalama wakimdhibiti mwandamanji nje ya makao ya rais nchini Sri Lanka.
Walinda usalama wakimdhibiti mwandamanji nje ya makao ya rais nchini Sri Lanka. AP - Eranga Jayawardena
Matangazo ya kibiashara

Japokuwa marshati hayo ya dharura hayakuwekwa wazi kwa umma, sheria za awali za hali ya dharura nchini humo zinampa nguvu rais kutuma vikosi vya jeshi kuwakabili wanaandamanji, kuwakamata na kuwazuia bila ya kufunguliwa mashataka.

Taarifa kutoka kwa ofisi ya rais kwenye taifa hilo imesema kuwa, agizo hilo limetolewa kwa ajili ya kuimarisha na kulinda usalama wa raia, kuzuia machafuko pamoja na kuhakikisha usambazaji wa bidhaa muhimu kwa raia unawafikia bila ya changamoto.

Tangazo hili la rais Rajapaksa, limekashifiwa vikali na upinzani nchini Sri Lanka pamoja na mataifa ya magharibi, balozi wa Marekani nchini humo Julie Chung kupitia mtandao wake wa kijamii wa twita akionyesha kughadhabishwa na agizo hilo.

Ijuma ya wiki, maofisa wa polisi waliwatawanya wa mabomu ya machozi waandamanji waliokuwa wamekusanyika nje ya majengo ya bunge, maandamano ya hivi punde dhidi ya serikali ya rais Gotabaya kutokana na upungufu wa bidhaa muhimu zinazoingizwa kwenye taifa hilo ikiwemo mafuta ya petrol, dawa pamoja na vyakula.

Shirika ya kutetea haki za watoto katika umoja wa mataifa UNICEF, limesema watoto walikuwa miongoni wa watu waliorushiwa mabomu ya machozi yaliorushwa na maofisa wa polisi.

Sri Lanka, tayari imeomba msaada wa kifedha kutoka kwa shirika la fedha duniani IMF ambapo serikali inatarajiwa kufanya kikao na IMF kupitia njia mtandao siku ya jumatatu ya wiki ijayo.

Taifa hilo limekumbwa na changamoto za kiuchumi baada yake kutatizika pakubwa na msambao wa Uviko 19 pamoja na kupanda kwa bei ya mafuta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.