Pata taarifa kuu

Jeshi la Ukraine ladai kuwa Urusi limeshambulia bila mafanikio Donbass

Vikosi vya Urusi vimeshambulia jimbo la Donbass mashariki mwa Ukraine leo Jumamosi, na kushindwa kufikia malengo yake matatu, jeshi la Ukraine limesema.

Silaha ya kivita wakati wa mafunzo mnamo Januari 2022 kabla ya vita vya Ukraine.
Silaha ya kivita wakati wa mafunzo mnamo Januari 2022 kabla ya vita vya Ukraine. © Russian Defense Ministry Press Service/AP
Matangazo ya kibiashara

Urusi imejaribu kuteka maeneo ya Lyman huko Donetsk na Sievierodonetsk na Popasna huko Luhansk, makao makuu ya jeshi la Ukraine yamesema wakati wa mkutano wake wa kila siku. "Bila mafanikio katika mashambulizi yake- mapigano yanaendelea," jeshi limesema.

Kulingana na taarifa za ujasusi kutoka Ukraine, kufanyika kwa  "kura ya maoni" kwa minajili ya kutangazwa kuanzishwa kwa "jamhuri" katika mkoa wa Kherson wa Ukraine kunaweza kupingwa na raia kutoka sehemu mbalimbali.

Urusi ilisema siku ya Jumamosi vitengo vyake vya mizinga vimelenga maeneo 389 ya jeshi la Ukraine usiku waIjumaa kuamkia leo Jumamosi, ikiwa ni pamoja na vituo 35 vya ukaguzi, ghala 15 za silaha na risasi na maeneo kadhaa ambapo wanajeshi na vifaa vya Ukraine vimewekwa. Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema makombora yake yaligonga maghala manne ya risasi na mafuta. Madai ambayo hayajathibitishwa na vyanzo huru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.