Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Urusi yatoa wito kwa NATO kuacha kuipatia Ukraine silaha

Katika siku ya 66 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Aprili 30, Sweden imetangaza uimarishaji wa miundombinu yake ya kijeshi kwenye kisiwa cha Gotland. Wakati Pentagon imetaja kutozingatia ukatili kama huo kutoka kwa jeshi la Urusi na Vladimir Putin kabla ya vita.

Wanajeshi wa Ukraine katika mkoa wa Donetsk, Aprili 28, 2022.
Wanajeshi wa Ukraine katika mkoa wa Donetsk, Aprili 28, 2022. REUTERS - SERHII NUZHNENKO
Matangazo ya kibiashara

Urusi ilisema siku ya Jumamosi vitengo vyake vya mizinga vimelenga maeneo 389 ya jeshi la Ukraine usiku waIjumaa kuamkia leo Jumamosi, ikiwa ni pamoja na vituo 35 vya ukaguzi, ghala 15 za silaha na risasi na maeneo kadhaa ambapo wanajeshi na vifaa vya Ukraine vimewekwa. Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema makombora yake yaligonga maghala manne ya risasi na mafuta. Madai ambayo hayajathibitishwa na vyanzo huru.

Kituo cha mafuta katika eneo la Bryansk nchini Urusi kimeshambuliwa kwa makombora, vyombo vya habari vya Urusi vimeripoti.

Huko Kharkiv, milipuko mikali ilitokea usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov anahimiza NATO na Marekani kuacha kuwasilisha silaha kwa Ukraine, ikiwa "wana nia ya kutatua mgogoro wa Ukraine".

Uingereza hivi karibuni itatuma timu ya wataalamu kusaidia wachunguzi wa Ukraine na kimataifa katika uchunguzi wao kuhusu ukatili uliofanywa tangu uvamizi wa Urusi, alitangaza Ijumaa Waziri wa Mambo ya Nje akizuru Uholanzi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema Ijumaa kwamba kuna hatari kubwa mazungumzo ya amani na Moscow yasitishwe.

Watu milioni 1.02 "wamehamishwa" kutoka Ukraine hadi Urusi tangu Februari 24, amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov. Kulingana na Kyiv, maelfu ya Waukraine "wamefukuzwa" na Moscow.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.