Pata taarifa kuu

Ukraine yafutilia mbali hoja ya kuwekwa kwa maeneo ya usalama wa kiutu Azovstal

Kwa siku ya 61 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Aprili 25, mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi wa Marekani wamekutana huko Kyiv na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Kiwanda cha Azovstal katika jiji la bandari la Mariupol mnamo Aprili 22, 2022.
Kiwanda cha Azovstal katika jiji la bandari la Mariupol mnamo Aprili 22, 2022. © ALEXANDER ERMOCHENKO/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri hao wa Marekani wametangaza kurejea hatu kwa hatua kwa wanadiplomasia wa Marekani nchini Ukraine na kutolewa kwa misaada mipya ya kijeshi. Wakati huo huo Mamlaka ya Urusi imetangaza kusitisha mapigano siku ya Jumatatu huko Mariupol.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken pamoja na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin walikuwa mjini Kyiv siku ya Jumapili , ambako walikutana na Rais wa Ukraine. Walitangaza kurejea hatu kwa hatua kwa wanadiplomasia wa Marekani nchini Ukraine na msaada mpya wa kijeshi, wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja, wa dola milioni 700. Siku ya Jumapoili mchana Rais Biden alithibitisha kwamba anataka kumteua Bridget Brink kama balozi wa Marekani nchini Ukraine.

Mashambulizi ya anga na milipuko ilifanyika usiku katika maeneo ya Vinnytska, Lviv nchini Ukraine. Nchini Urusi, moto ulizuka katika ghala za mafuta huko Bryansk, kilomita 150 kutoka mpaka wa Ukraine.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, anatarajiwa Jumatatu hii nchini Uturuki, nchi ambayo inajaribu kupatanisha mgogoro wa Ukraine. Baadae ataenda Moscow na kisha Kyiv.

Ukraine inapendekeza mazungumzo na Urusi karibu na jengo kampuni kubwa ya madini ya Azovstal huko Mariupol (kusini-mashariki), ambapo wapiganaji wa Ukraine na raia bado wamejikita katika mji ambao kwa kiasi kikubwa uko chini ya udhibiti wa Urusi, ofisi ya rais wa Ukraine ilitangaza siku ya Jumapili.

Moscow imetangaza kusitisha mapigano Jumatatu ili kuruhusu raia kuondoka katika kiwanda cha Azovstal. Umoja wa Mataifa ulitoa wito siku ya Jumapili kuwepo kwa makubaliano ya "mara moja" huko Mariupol, ili kuruhusu kwa upana zaidi uhamisho wa raia 100,000 ambao bado wamekwama katika bandari hii ya Ukraine inayodhibitiwa kabisa na jeshi la Urusi.

Idadi ya wakimbizi wanaokimbia uvamizi wa Urusi inazidi milioni 5.2, kulingana na Umoja wa Mataifa. Zaidi ya watu milioni 7.7 wametoroka nyumba zao lakini bado wako Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.