Pata taarifa kuu

Ukraine: Umoja wa Mataifa watoa wito wa kusitishwa 'haraka' kwa mapigano Mariupol

Umoja wa Mataifa umetoa wito Jumapili hii kwa makubaliano ya kusitisha mapigano "mara moja" huko Mariupol, ili kuwezesha zoezi la kuhamisha raia uhamisho wa raia 100,000 ambao bado wamekwama katika bandari hii ya Ukraine inayodhibitiwa kabisa na jeshi la Urusi.

Vifaru vya Urusi vikiwa barabarani katika eneo linalodhibitiwa na vikosi vilivyojitenga vinavyoungwa mkono na Urusi huko Mariupol, Ukraine, Jumamosi, Aprili 23, 2022.
Vifaru vya Urusi vikiwa barabarani katika eneo linalodhibitiwa na vikosi vilivyojitenga vinavyoungwa mkono na Urusi huko Mariupol, Ukraine, Jumamosi, Aprili 23, 2022. AP - Alexei Alexandrov
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken anatarajiwa mjini Kyiv Jumapili hii, taarifa ambazo hazijathibitishwa kwa upande wa Marekani.

Idadi ya wakimbizi wanaokimbia uvamizi wa Urusi inakaribia kufikia milioni 5.2, kulingana na Umoja wa mataifa. Zaidi ya watu milioni 7.7 wameyotoroka nyumba zao lakini bado wako nchini Ukraine.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres atasafiri kwenda Urusi Jumanne tarehe 26 Aprili ambapo atapokelewa na Vladimir Putin. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa afisa huyo wa Umoja wa Mataifa kupokelewa na mamlaka ya Urusi tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine tarehe 24 Februari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.