Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Zelensky adai watu 3,000 'waliokolewa' kutoka Mariupol

Katika siku ya 38 ya uvamizi wa Ukraini na Urusi, Jumamosi hii Aprili 2, fuata taarifa zetu za hivi punde moja kwa moja.

Wakimbizi kutoka mji uliozingirwa wa Mariupol wakipowasili Zaporizhia mnamo Aprili 1, 2022.
Wakimbizi kutoka mji uliozingirwa wa Mariupol wakipowasili Zaporizhia mnamo Aprili 1, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Zaidi ya watu 3,000 "wameokolewa" kutoka Mariupol, mji wa kusini mashariki mwa Ukraine uliozingirwa na vikosi vya Urusi, amesema Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika video iliyotolewa usiku wa Ijumaa hadi Jumamosi.

► Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) inasema imelazimika kusitisha zoezi lake baada ya hali kuona kuwa "haitowezekana kuendelea na zoezi" la uhamishaji kutoka Mariupol. Timu za ICRC zitajaribu tena Jumamosi "kuwezesha kupita kwa usalama kwa raia kutoka Mariupol", mji unaozingirwa na kushambuliwa kwa makombora tangu mwisho wa mwezi Februari na vikosi vya Urusi na ambapo raia 160,000 bado wanaaminika wamekwama katika mji huo.

► Pentagon imetangaza hadi dola milioni 300 kama msaada wa ziada wa kijeshi kwa Ukraine.

Katika mji wa Kyiv, majengo 154 ya makazi, bustani 20 za kibinafsi, shule za chekechea 27 na shule 44 zimeharibiwa tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi, kulingana na manispaa ya jiji la mji mkuu kwenye ukurasa wake wa Telegraph.

Zaidi ya maduka 760 ya vyakula na mikahawa 400 bado yanafanya kazi.

Katika tangazo la video usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema: "Wavamizi wameanza kurudi nyuma kaskazini mwa nchi.

Wanajeshi wa Urusi waelekea Donbass na Kharkiv. Wanajiandaa kwa kutekeleza mashambulizi makubwa, tunajiandaa kwa kujihami na mashambulizi hayo, amesema Rais Zelensky.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.