Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Angalau 1351 wauawa katika safu ya jeshi la Urusi

Katika siku ya 30 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, nchi za Magharibi zakubaliana kupunguza utegemezi wa Ulaya kwa gesi na mafuta kutoka Urusi. Rais wa Marekani Joe Biden amewasili nchini Poland. Watoto milioni 4.3 wa Ukraine wamekimbia makazi yao na jeshi la Urusi linakiri kuuawa kwa wanajeshi 1,351 katika safu yake.

Majengo yaliyoharibiwa katika mji wa Bucha, karibu na mji mkuu wa Kyiv, Ukraine, Jumanne, Machi 1, 2022.
Majengo yaliyoharibiwa katika mji wa Bucha, karibu na mji mkuu wa Kyiv, Ukraine, Jumanne, Machi 1, 2022. AP - Serhii Nuzhnenko
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Jeshi la Urusi linakiri kupoteza wanajeshi 1,351 tangu kuanza kwa vita  nchini Ukraine mwezi mmoja uliopita.

► Zaidi ya nusu ya watoto wa Ukraine wamekimbia makazi yao baada ya mwezi mmoja wa vita, yaani watoto milioni 4.3, na raia milioni 10 wa Ukraine wamekimbia makazi yao kulingana na Umoja wa Mataifa.

► Hali katika jiji lililozingirwa la Mariupol, kusini mwa nchi, kwenye Bahari ya Azov, inazidi kuwa mbaya, Waukraine wanashutumu idadi kubwa ya wakazi wa mji huo kwenda Urusi. Hlamshauri ya Manispaa ya jiji inakadiria kuwa karibu watu 300 walikufa katika shambulio la bomu dhii ya ukumbi wa michezo.

► Makubaliano kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani yanafaa kutiwa saini ili kuruhusu Wamarekani kusambaza gesi asilia iliyoyeyushwa zaidi kwa Umoja wa Ulaya. Ujerumani itaweza kufanya hivyo bila makaa ya mawe kutoka Kirusi ifikapo msimu wa joto mwaka huu.

Wakati huo huo ndege ambayo Rais wa Poland Andrzej Duda alikuwa akisafiri kuelekea mashariki mwa Poland kukutana na mwenzake wa Marekani Joe Biden ilitua kwa dharura baada ya kurejea Warsaw, anasema mshauri wa rais, Jakub Kumoch, aliyenukuliwa na shirika la habari la PAP. Pawel Szrot, mkurugenzi katika ofisi ya rais, Andrzej Duda, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba rais wa Poland yuko salama salimini.

Urusi inakiri kuuawa kwa wanajeshi wake 1,351 tangu kuanza kwa mashambulizi yake ya kijeshi nchini Ukraine mwezi mmoja uliopita, ikizishutumu nchi za Magharibi kwa kufanya "kosa" kwa kuipa silaha Kyiv. "Wakati wa operesheni maalum ya kijeshi, askari 1,351 waliuawa na 3,825 kujeruhiwa," Naibu Mkuu wa jeshi la Urusi Sergei Roudskoy amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.