Pata taarifa kuu

Ukraine: NATO yakutana kwa mazungumzo kuhusu hatua za kukabiliana na vita vya Moscow

Katika siku ya 29 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, watoto milioni 4.3 wa Ukraine wamelazimika kuyahama makazi yao. Mikutano mitatu (G7, NATO, Baraza la Ulaya) imepangwa mjini Brussels na nchi za Magharibi zinakusudia kuimarisha hatua vikwazo dhidi ya Urusi ili kuendelea kwa muda mrefu. Vikosi vya Urusi bado vinauzingira mji mkuu wa bandari wa kusini wa Mariupol, unaoelezewa kuwa "kuzimu ya kibinadamu".

Rais wa Marekani Joe Biden, katikati, akiwasili kwa mjadala wa jopo wakati wa Mkutano wa dharura wa NATO kwenye Makao Makuu ya NATO huko Brussels, Alhamisi, Machi 24, 2022.
Rais wa Marekani Joe Biden, katikati, akiwasili kwa mjadala wa jopo wakati wa Mkutano wa dharura wa NATO kwenye Makao Makuu ya NATO huko Brussels, Alhamisi, Machi 24, 2022. AP - Markus Schreiber
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wakuu wa Magharibi wamekubaliana kuimarisha Ulinzi mpakani na Urusi kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

"Tumeanzisha mipango ya ulinzi ya NATO, tumepeleka kikosi cha Nato, na kuweka wanajeshi 40,000 kwenye eneo letu upande wa mashariki," Viongozi hao waMEtangaza katika taarifa ya pamoja baada ya mazungumzo huko Brussels.

Wakati huohuo, jeshi la wanamaji la Ukraine limesema limeharibu meli ya Urusi katika mji wa bandari wa Berdyansk wa Ukraine unaokaliwa kwa mabavu.

Uingereza imetangaza vikwazo vipya dhidi ya watu na mashirika 65 zaidi ya Urusi, likiwemo Kundi la mamluki la Wagner.

Pointi kuu:

► Zaidi ya nusu ya watoto wa Ukraine wamekimbia makazi yao baada ya mwezi mmoja wa vita, sawa na watoto milioni 4.3, kulingana na Umoja wa Mataifa. Waukraine milioni 10 wamekimbia makazi yao.

► Alhamisi hii, mataifa ya Ulaya na Amerika Kaskazini yanakutana Brussels kwa mikutano mitatu: ule wa NATO asubuhi na ule wa G7 na Baraza la Ulaya mchana. Joe Biden aliwasili jana usiku katika mji mkuu wa Ubelgiji kushiriki katika mikutano hiyo. Kisha atasafiri kwenda Poland.

► Wanajeshi wa Urusi bado wanajaribu, bila mafanikio, kuzunguka kyiv. Baadhi ya maeneo ya makazi ya mji mkuu yalilengwa na mashambulizi ya anga ya siku ya Jumatano. Mashambulio ya anga ya majeshi ya Urusi yanaendelea katika miji mingi ya Kiukreni, kama vile Kharkiv, Mariupol, Odessa, Mykolaiv, lakini bila maendeleo makubwa ya kimkakati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.