Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Volodymyr Zelensky kulihutubia Bunge la Ufaransa

Siku ya 28 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumatano Machi 23, vikosi vya Urusi havidhibiti kyiv wala mji mkubwa wa bandari wa Mariupol, ambao umezingirwa kwa wiki kadhaa. Bunge la Ufaransa linasubiri hotuba ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kupitia njia ya video.

Mwanajeshi wa Ukraine katika eneo la Uhuru huko Kyiv, Jumatano Machi 23.
Mwanajeshi wa Ukraine katika eneo la Uhuru huko Kyiv, Jumatano Machi 23. AFP - SERGEI SUPINSKY
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Wanajeshi wa Urusi bado wanajaribu, bila mafanikio, kuzingira mji wa Kyiv. Baadhi ya maeneo ya makazi ya mji mkuu yamelengwa na mashambulizi ya anga ya Urusi siku ya Jumatano. Mashambulizi ya anga ya Urusi yanaendelea katika miji mingi ya Ukraine, kama vile Kharkiv, Mariupol, Odessa, Mykolaiv, lakini bila maendeleo makubwa ya kimkakati.

► Kyiv na Moscow kila upane moja umeelezea kuwa mazungummzo na Urusi kuwa "magumu" , mazungumzo yaliyofanyika kwa nia ya kusitisha uhasama, pande hizo mbili zikikataa kuwajibika kwa vizuizi. Baada ya duru kadhaa za mazungumzo ya ana kwa ana, na ambayo yanaendelea mtandaoni, amesema kiongozi wa ujumbne wa Ukraine katika mazungumzo.

► Rais wa Ukraine atazungumza kwa njia ya video na wwabunge wa Ufaransa Jumatano hii, Machi 23 kuanzia saa tatu usiku saa za Afrika ya Mashariki ili kupata uungwaji mkono zaidi kutoka kwa Ufaransa katika kukabiliana na vita vinavyoendeshwa na Urusi. Mapema siku ya Jumatano, alihutubia bunge la Japan, akitaka mageuzi ya Umoja wa Mataifa.

► Joe Biden anawasili Ulaya ambapo atashiriki katika mkutano wa kilele wa NATO, G7 na Umoja wa Ulaya siku ya Alhamisi kabla ya kwenda Poland.

► Volodymyr Zelensky alisema katika video iliyotolewa Jumanne jioni kwamba watu 100,000 wanaishi katika Mariupol iliyozingirwa katika "hali isiyo ya kibinadamu". Mamlaka imetangaza juhudi mpya za kujaribu kuwahamisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.