Pata taarifa kuu

Ukraine: NATO yajipanga dhidi ya shambulio la nyuklia, kemikali au kibaolojia

NATO itaipa Ukraine vifaa vya kujikinga dhidi ya vitisho vya kemikali, kibaiolojia na nyuklia na italinda vikosi vyake vilivyotumwa kwenye upande wa mashariki dhidi ya vitisho hivi, Katibu Mkuu wa Muungano ametangaza Alhamisi Machi 24.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg (kushoto) akiwa na Rais wa Marekani Joe Biden Machi 24, 2022.
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg (kushoto) akiwa na Rais wa Marekani Joe Biden Machi 24, 2022. AP - Thibault Camus
Matangazo ya kibiashara

Washirika wana "wasiwasi" juu ya uwezekano wa matumizi ya silaha kama hizo nchini Ukraine baada ya uvamizi wa Urusi na "wamekubali kutoa vifaa vya kusaidia Ukraine kujilinda dhidi ya vitisho vya kemikali, kibaolojia, radiolojia na nyuklia", amesema Jens Stoltenberg mwishoni mwa mkutano wa dharura wa viongozi wa jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi. "Inaweza kuwa kugundua, vifaa, ulinzi na usaidizi wa kimatibabu, pamoja na mafunzo kwa maambukizi yoyote na udhibiti wa mgogoro," amesema.

 

"Pia tunaboresha utayari wa vikosi vya washirika. Kamanda Mkuu wa Vikosi vya kijeshi vya Muungano, Jenerali Walters, amezindua vitengo vya ulinzi vya NATO vya kemikali, baiolojia, radiolojia na nyuklia na washirika wetu wanapeleka uwezo wa ulinzi ili kuimarisha vikosi maalumu katika masuala ya vita", ameongeza. "Kwa hivyo tunachukua hatua kuunga mkono Ukraine na kujilinda," amesema.

Muhula wa Stoltenberg waongezwa kwa mwaka mmoja

Washirika wamekubali kufanya zaidi kuisaidia Ukraine baada ya kusikia Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akisisitiza "umuhimu wa kutoa msaada zaidi wa kijeshi kwa nchi yake", amesema Jens Stoltenberg, aliyeongezwa tena muhula kwa mwaka mmoja. Hakutaja ni silaha gani zitatolewa na washirika, lakini Marekani "imeanza mashauriano ya kutoa makombora ya kukinga meli kwa Ukraine", afisa mkuu wa Marekani amesema wakati wa mkutano huo.

Viongozi wa Muungano pia wameidhinisha kuundwa kwa vitengo maalumu vingine vinne vya masuala ya kivita huko Romania, Hungary, Bulgaria na Slovakia, na kuimarisha vitengo vinne ambavyo tayari vimeundwa huko Poland na nchi tatu za Baltic.

Zaidi ya wanajeshi 100,000 wa Marekani kwa sasa wako Ulaya na zaidi ya wanajeshi 40,000 wako chini ya amri ya moja kwa moja ya NATO katika sehemu ya mashariki ya Muungano huo, Jens Stoltenberg amesema.

Viongozi wa Muungano wataamua, wakati wa mkutano wao wa kilele mwishoni mwa Juni huko Madrid, juu ya marekebisho ya ulinzi wao. Majadiliano yatazingatia uendelevu wa vikosi hivi na ongezeko la matumizi ya kijeshi ya Washirika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.