Pata taarifa kuu

Volodymyr Zelensky mbele ya Bunge la Italia aomba vikwazo zaidi dhidi ya Urusi

Kwa muda wa dakika 11, Volodymyr Zelensky ameelezea hali ya Ukraine na kutoa upya wito wake wa usaidizi kutoka kwa nchi za Umoja wa Ulaya na G7. Ombi ambalo kiongozi wa serikali ya Italia Mario Draghi amejibu, akiahidi kuimarisha misaada kutoka Italia, ikiwa ni pamoja na kijeshi.

Wabunge wa Italia wakisikiliza hotuba ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Machi 22, 2022.
Wabunge wa Italia wakisikiliza hotuba ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Machi 22, 2022. © Remo Casilli/Pool via AP
Matangazo ya kibiashara

"Fikirieni Genoa imeharibiwa kabisa baada ya wiki kadhaa za mashambulizi ya anga". Ni kwa maneno hayo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewatahadharisha wabunge wa Italia kuhusu uharibifu wa mji wa Mariupol, mji ulioko kusini mashariki mwa Ukraine unaozingirwa na kushambuliwa kwa mabomu na majeshi ya Urusi, akiufananisha na mji mkubwa wa Italia wa Genoa.

Rais wa Ukraine amekumbusha hasa kwamba watoto 117 wameuawa tangu kuanza kwa mashambulio ya Urusi yaliyozinduliwa mnamo Februari 24, kulingana na hesabu ya ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Ukraine.

Baada ya vita kutangazwa "watu wetu wamekuwa jeshi letu na ngome ya Ulaya", ameishukuru Italia kwa kuwa kuwapokea zaidi ya wakimbizi 60,000. Lakini Volodymyr Zelensky ameomba vikwazo zaidi.

Tangu uvamizi wa Ukraine na Urusi, Volodymyr Zelensky hajaacha kuziomba nchi za magharibi waimarishe hatua zinazochukuliwa dhidi ya Moscow ili kumaliza vita nchini mwake na kuepusha athari za mzozo huo sehemu nyingine duniani.

Akiwahutubia wabunge wa Italia, amewakashifu bila kuwataja kuhusiana na "ucheleweshaji" wa nchi za Magharibi katika "shinikizo lililowekwa kwa Urusi".

Maneno ya rais wa Ukraine yamepongeza kwa muda mrefu na kufuatiwa na hotuba ya Waziri Mkuu Mario Draghi ambaye amesifu ujasiri wa Waukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.