Pata taarifa kuu

[Moja kwa moja] Vita nchini Ukraine: EU yaamua kuzuia mali za Putin na Lavrov

Katika siku ya pili ya mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine, Kiev inakabiliwa na mashambulizi ya kombora na mapigano yanaendelea kaskazini mwa mji mkuu wa Ukraine, huku wanajeshi wa Urusi wakikusanyika katika mji huo kutoka kaskazini, kaskazini mashariki na mashariki mwa Ukraine.

Magari ya kijeshi yaliyoharibiwa kwenye barabara huko Kharkiv, Februari 25, 2022.
Magari ya kijeshi yaliyoharibiwa kwenye barabara huko Kharkiv, Februari 25, 2022. © REUTERS/Maksim Levin
Matangazo ya kibiashara

Mkutano wa kilele wa NATO utafanyika Ijumaa hii kwa njia ya video. Umoja wa Ulaya umeamua kuzuia mali katika za Vladimir Putin na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov katika nchi wanachama wa Umoja huo.

Mambo muhimu:

► Ijumaa hii, macho yameelekezwa kwenye mji mkuu Kiev, unaokabiliwa na mashambulizi yamakombora na ambapo mapigano yanaendelea. Rais wa Ukraine amesema yeye ndiye "mlengwa namba moja" wa Moscow.

► Uhamasishaji wa jumla umeamuliwa kwa upande wa Ukraine. Rais wa Ukraine alitoa idadi ya muda ya vifo vya watu 137 na 316 waliojeruhiwa katika mapigano Alhamisi jioni. Aidha,  Watu walioyahama makazi yao wanafikia 100,000 kulingana na Umoja wa Mataifa, na watu 50,000 tayari wameitoroka nchi.

► Vikwazo vingi vimechukuliwa na Umoja wa Ulaya, lakini pia Marekani, Uingereza na Canada zikilenga sekta ya benki, uagizaji wa bidhaa za kiteknolojia na wale walio karibu na mamlaka. Umoja wa Ulaya umeamua kuzuia mali za Vladimir Putin na Sergei Lavrov katika nchi wanachama wa umoja huo.

► Mkutano wa kilele wa NATO unafanyika Ijumaa hii kwa mkutano wa video. Marekani italinda "eneo la NATO", lakini haitatuma wanajeshi wake Ukraine, ametangaza rais wa Marekani Joe Biden. Marekani imeamuru wanajeshi 7,000 wa ziada kwenda Ulaya.

► Mataifa ya Magharibi yameongeza vikwazo vya kifedha kwa benki za Urusi na maafisa wa ngazi za juu, huku Marekani ikikata mauzo ya teknolojia ya juu nchini Urusi - lakini mataifa ya Nato hayatatuma wanajeshi wake Ukraine.

► Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameapa kuendelea na mapigano, akisema kuwa "pazia jipya la chuma" linaangukia mahali pake - na kazi yake ni kuhakikisha nchi yake inasalia upande wa magharibi.

► Maandamano ya kupinga vita na maandamano ya kuunga mkono Ukraine yamefanyika katika miji kote Ulaya - na pia nchini Urusi, licha ya ukandamizaji ambao umesababisha kukamatwa kwa watu zaidi ya 700.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.