Pata taarifa kuu

Ukraine: Umoja wa Ulaya waidhinisha "kwa kauli moja" vikwazo dhidi ya Urusi

Baada ya uamuzi wa Moscow wa kutambua maeneo yaliyotangaza kujitenga mashariki mwa Ukraine, nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya "kwa kauli moja" zimeidhinisha "vikwazo" siku ya Jumanne, ametangaza waziri wa Ufaransa wa Mambo ya Nje Jean-Yves Le Drian.

Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Moscow, Oktoba 13, 2021.
Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Moscow, Oktoba 13, 2021. AP - Mikhail Metzel
Matangazo ya kibiashara

"Tumekubaliana kwa kauli moja juu ya kifurushi cha kwanza cha vikwazo" ametangaza ametangaza Waziri wa Mmabo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian baada ya mkutano wa mawaziri 27 wa mambo ya nje huko Paris.

Vikwazo hivi "vitaumiza sana Urusi", amehakikishia Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell.

Hayo yanajiri wakati rais wa Urusi Vladimir Putin ameagiza jeshi la Urusi "kulinda amani" katika maeneo yaliyojitenga.

Sheria mbili za rais wa Urusi zinaomba Wizara ya Ulinzi kwamba vikosi vya jeshi vya Urusi vichukue "kazi za kulinda amani kwenye eneo" la jamhuri za watu za Donetsk na Lugansk. Hatua moja zaidi kuelekea kuongezeka kwa uhasama usiokoma.

Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo, wanajeshi wa Urusi tayari wameanza kupelekwa katika maeneo hayo, magari ya kijeshi na magari ya kivita yanaelekea Donbass na baadhi tayari yapo kwenye mitaa ya Donetsk.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.