Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron kulihutubia Bunge la Ulaya Strasbourg

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atalihutubia Jumatano hii, Januari 19, Bunge la Ulaya mjini Strasbourg kuelezea vipaumbele vya uenyekiti wa Ufaransa kwa Umoja wa Ulaya.

Emmanuel Macron anatarajiwa katika Bunge la Ulaya saa 11:20 mchana kuzindua uenyekiti wa Ufaransa kwa Umoja wa Ulaya, Januari 19, 2022.
Emmanuel Macron anatarajiwa katika Bunge la Ulaya saa 11:20 mchana kuzindua uenyekiti wa Ufaransa kwa Umoja wa Ulaya, Januari 19, 2022. JOHN THYS POOL/AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Kipindi cha maswali na majibu kitafuata katika jengo hilo la Bunge kati ya rais Emmanuel Mcron, kama mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya na wabunge wa umoja huo. 

Miezi mitatu kabla ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa, zoezi hilo linatarajia kugeuza sura na  kuwa mzozo wa kisiasa kwa Ufaransa. Tukio hili ambalo halijawahi kushuhudiwa linatoa nafasi kwa mkuu wa nchi na wapinzani wake.

Marine Le Pen ndiye alifungua sherehe hizo jana kwa mkutano na waandishi wa habari mjini Paris. Miaka mitano baada ya kushindwa katika uchaguzi wa urais, mgombea huyo wa siasa kali za mrengo wa kulia amerekebisha hotuba yake ili kuwafurahisha watu wengi iwezekanavyo

Kama Marine Le Pen, Jean-Luc Mélenchon pia alizua mtafaruku. Mnamo mwaka 2017, alitaka "Ufaransa kuondoka kwenye mikataba ya Ulaya". Mnamo mwaka 2022, anapendelea "kutotii" baadhi ya sheria za Ulaya.

Jean-Luc Mélenchon na Yannick Jadot katika mkutano

Jean-Luc Mélenchon alielezea mpango wake wa Ulaya jana huko Strasbourg ambapo atafanya mkutano Jumatano jioni, sambamba na Yannick Jadot. Kwa sababu yeye ni mbunge, mwanaikolojia huyo ndiye mgombea pekee wa urais ambaye ataweza kupambana na Emmanuel Macron moja kwa moja Bungeni. Kama mkuu wa nchi, anaonekana kuunga mkono Ulaya na shirikisho, huku akikosoa sana mikataba ya biashara huria au sera ya hali ya hewa ya Tume ya Ulaya

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.