Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Emmanuel Macron ajiandaa kushiriki katika kinyang'anyiro cha urais

"Ufaransa inaelekea wapi" kilikuwa kichwa cha makala ya televisheni ya TF1 na LCI wakati Emmanuel Macron alijibu maswali kutoka kwa wanahabari wawili kwa karibu saa mbili Jumatano, Desemba 15.

Emmanuel Macron wakati wa kipindi cha televisheni "Ufaransa inaelekea wapi", Desemba 15, 2021.
Emmanuel Macron wakati wa kipindi cha televisheni "Ufaransa inaelekea wapi", Desemba 15, 2021. Ludovic MARIN AFP
Matangazo ya kibiashara

Swali kubwa ilikuwa kujua zaidi ni wapi Emmanuel Macron anaenda? Rais hakusema kuwa atawania katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwaka 2022 bali alionesha kuwa anajiandaa kwa ajili ya kuingia kwenye kampeni za urais.

Ikiwa sio mgombea, inaonekana kama hivyo. Akirejea kwenye matokeo ya muhula wake wa miaka mitano, Emmanuel Macron alibainisha hatua ya kwanza muhimu kwa rais anayemaliza muda wake ambaye anataka kuchaguliwa tena: kusema kile alichokifanya vizuri, kujitahidi, kile ambacho hakuweza kufanya, hakuweza kubainisha wazi.

Na ujumbe wake ulikuwa wazi: "Nilijifunza" unyenyekevu, heshima, kupenda Wafaransa. Majibu mengi kwa shutuma zote ambazo anaweza kuwa alikumbana nazo juu ya kupingwa kwake, kiburi chake; kama jaribio la kumwondoa mhusika kwenye taswira yake kabla ya kuingia undani wa kampeni na kujaribu kuwachokonoa wapinzani wake.

Wapinzani anaopambana nao katika kinyang'anyiro hiki, lakini bila kuwataja ni Valérie Pécresse na hasa Eric Zemmour.

Na kisha, Emmanuel Macron alionyesha maono yake ya Ufaransa, nia yake kamili ya kufanya mageuzi, hasa suala la pensheni. Na amesema nia yake ya kwenda mbali zaidi. Mara nyingi alitumia neno "sisi" kumaanisha Wafaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.