Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Kansela Scholz na Rais Macron waahidi kuendeleza ushirikiano wa karibu

Kansela mpya wa Ujerumani Olaf Scholz, anayezuru Paris, na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wameonesha Ijumaa hii, Desemba 10, "muunganisho" wao wa maoni juu ya Ulaya. Pia wameonyesha nia yao ya "kufanya kazi pamoja" katika kukabiliana na changamoto kubwa za kimataifa.

Kansela mpya wa Ujerumani, Olaf Scholz, alikutana na Rais Emmanuel Macron Ijumaa hii, Desemba 10 mjini Paris.
Kansela mpya wa Ujerumani, Olaf Scholz, alikutana na Rais Emmanuel Macron Ijumaa hii, Desemba 10 mjini Paris. AP - Thibault Camus
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia utamaduni wa muda mrefu wa baada ya vita, Olaf Scholz, ambaye alimrithi Angela Merkel mnamo Jumatano, Desemba 8, anazuru Paris mara tu masuala ya kwanza ya ndani yalipochukuliwa huko Berlin. Kansela na Rais, ambao tayari wanfahamiana, haraka wamejadili masuala mbalimbali, kuanzia Umoja wa Ulaya (EU) hadi mgogoro wa Ukraine.

"Mazungumzo haya ya kwanza yanaonyesha wazi muunganiko wa maoni thabiti", amekaribisha Emmanuel Macron wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari. Olaf Scholz amebainisha "njia nyingi za kujenga" kwa kuzingatia uenyekiti wa Ufaransa kwa Umoja wa Ulaya na Ujerumani kwa mataifa yaliyostawi kiviwanda, G7, mwaka 2022. "Nina hakika kwamba uhusiano wa Ufaransa na Ujerumani utaendelea kustawi", ameongeza.

Rais Macron amesema yeye na mgeni wake wamedhihirisha kuwa Ufaransa na Ujerumani zitaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu, kama ilivyokuwa wakati wa utawala wa Bi Merkel.

Mada kuu kwenye mkutano huo wa kwanza kati ya Macron na Scholz kama kansela wa Ujerumani, zilikua ushirikino barani Ulaya, mabadiliko ya tabianchi, wahamiaji na kuimarisha mfumo wa kidigitali. Kansela Scholz amesema Ujerumani itashirikiana na Ufaransa kuijenga Ulaya Imara.

Kansela Scholz anatarajia kwenda mjini Brussels kufanya mazungumzo na rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen , na Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.