Pata taarifa kuu
ITALIA-HAKI

Kesi ya Matteo Salvini, anayetuhumiwa kuzuia wahamiaji baharini yafunguliwa

Naibu waziri mkuu wa Italia na Waziri wa Mambo ya Ndani wa serikali ya Conte 1, Matteo Salvini, amefikishwa, Jumamosi hii, Oktoba 23, mbele ya mahakama ya Palermo kutokana na kuhusika kwake kwa kuizuia meli ya kunusuru wahamiaji kutia nanga kwa kipindi cha siku sita katika bandari ya taifa hilo mwezi Agosti 2019.

Matteo Salvini pamoja na wakili wake, siku ya kwanza ya kesi yake huko Palermo, Oktoba 23, 2021.
Matteo Salvini pamoja na wakili wake, siku ya kwanza ya kesi yake huko Palermo, Oktoba 23, 2021. REUTERS - ANTONIO PARRINELLO
Matangazo ya kibiashara

Na hii licha ya hali mbaya ya afya ya kimwili na akili ya wahamiaji 121 ambao bado walikuwa ndani ya meli hiyo kwa jumla ya wahamiaji 147 waliookolewa mwanzoni mwa mwezi huu katika pwani ya Libya.

Kesi hii inaweza kumdhoofisha Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Matteo Salvini. Anashutumiwa kwa "kuwateka nyara watu" kwa kuwa alizuia kwa kipindicha sikuka dhaa, meli ya shirika la kihisani la Open Arms, kutoka Uhispani, mwezi Agosti 2019. Na "kutotimiza majukumu yake" kwa kukataa kuonyesha bandari ya ambapo meli hiyo ingeliegesha, tangu wakati meli hiyo ilipoingia kwenye maji ya eneo la Italia.

Kiongozi wa chama kinachopinga wahamiaji alikuwa amekataa kwa siku sita kutoa ruhusa kwa meli ya shirika hilolisilo la kiserikali kutoak Uhispania kuegesha kwenye bandari, hiyo, meli ambayo ilitia nanga kwenye kisiwa kidogo cha Italia cha Lampedusa, kusini mwa Sicily, wakati hali ya afya ya wahamiaji waliokuemo kwenye melihiyo iliendelea kuwa mbaya. Wahamiaji waliruhusiwa kushuka tu kwa agizo la mahakama ya Sicily baada ya ukaguzi ndani ya meli ambao ulithibitisha kuwa wahamiaji wengi wana hali mbaya ya kiafya kwenye meli hiyo iliyojaa watu.

Matteo Salvini, 48, anakabiliwa na hatari ya kupigwa marufuku kushikilia wadhifa wowote katika Bunge na katika shirika lolote la umma. Lakini pia kufungwa hadi miaka kumi na tano jela. Anadai kuwa alifanya hivyo kwa maslahi ya Italia na kuwazuia wahamiaji wasiendelei kutumia pwani za Afrika kwa kuvuka hatari ya Bahari ya Mediterania ili waweze kuingia Ulaya, akisisitiza kuwa uamuzi huo uliidhinishwa na serikali ya wakati huo na Waziri mkuu Giuseppe Conte.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.