Pata taarifa kuu

Erdogan na Merkel wapongeza uhusiano wao "mzuri" licha ya "tofauti"

Wakati mazungumzo yanaendelea nchini Ujerumani kuunda muungano mpya na kumteua mrithi wake, Kansela Angela Merkel amefanya ziara yake ya mwisho ya kiserikali kwa rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Jumamosi, Oktoba 16.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akipokelewa na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan huko Villa Huber kabla ya mkutano wao huko Istanbul Oktoba 16, 2021.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akipokelewa na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan huko Villa Huber kabla ya mkutano wao huko Istanbul Oktoba 16, 2021. © Murad Sezer, Reuters
Matangazo ya kibiashara

Bila kukana tofauti zao nyingi, viongozi hao wawili wamependelea kusisitiza juu ya juhudi zao za kupata maelewano, hasa juu ya suala la uhamiaji.

Recep Tayyip Erdogan amebaini kwamba atamkosa Angela Merkel ambaye alikuwa naye kwa ukaribu. Katika mkutano wao wa mwisho wa pamoja na waandishi wa habari, rais wa Uturuki ametaka kuendelea na uhusiano wake na serikali mpya ya Ujerumani kwa kile alichokiita "kazi yetu iliyofanikiwa na Merkel". Alisifu "uongozi" wa Kansela na kusifu itikadi yake "ya kujenga" katika miaka 16 waliyokuwa pamoja.

Bila kushangaza, viongozi hao wawili wamerejelea kwenye makubaliano ya uhamiaji ya 2016, yaliyofikiwa kati ya Ankara na moja wa Ulaya,makubaliano ambayo yalijadiliwa na Angela Merkel.

Angela Merkel amehakikisha kwamba EU itaendelea kuunga mkono Uturuki, akikumbusha euro Bilioni 6 ambazo tayari zimetengwa kwa nchi hii kuisaidia kuwakaribisha zaidi ya Wasyria milioni 3.7 na wkubaini "ni muhimu" kusaidia Ankara katika vita vyake dhidi ya biashara ya binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.