Pata taarifa kuu
UHISPANIA

Uhispania: Mazungumzo mapya yaanza kati ya Madrid na waasi

Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez anatarajiwa huko Barcelona Jumatano kuanza mazungumzo, ingawa matarajio ya makubaliano bado ni ndoto.

Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez, wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Vilnius, Julai 8, 2021.
Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez, wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Vilnius, Julai 8, 2021. AP - Mindaugas Kulbis
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo ambayo Iyamesitishwa kwa mwaka mmoja na nusu, mazungumzo kati ya Madrid na wanaharakati wanaotaka kujitenga katika Jimbo la Catalonia yanaanza tena Jumatano hii, Septemba 15.

Lengo ni kutafuta njia ya kuondokana na mgogoro katika eneo hili lililotikiswa na jaribio la kujitenga mwaka 2017. Baada ya kuongezeka kwa mashaka, siku ya Jumatatu jioni Waziri Mkuu Pedro Sanchez alisema kuwa atafanya ziara hiyo huko Barcelona kwa mazungumzo haya. "Nimekuwa nikitetea mazungumzo [...], hitaji la kufungua ukurasa mpya" huko Catalonia, alisema kiongozi huyo wa Kisoshalisti.

Walakini, matarajio ya makubaliano ni madogo kwani msimamo wa serikali kuu na serikali ya Jimbo la Catalonia ya mwanaharakati mwenye msimamo wa wastani Pere Aragonès zinatofautiana.

"Ikiwa tunakabiliwa na mahitaji magumu, ni wazi kwamba mazungumzo hayatadumu kwa muda mrefu, " amesema Pedro Sanchez, na kuongeza kura maoni ya kujitawala itakuwa "kinyume cha katiba".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.