Pata taarifa kuu
UFARANSA-USALAMA

Ufaransa: E. Macron ataka kuimarisha idara ya polisi kwa miaka 10

Rais wa Ufaransa alitangaza mageuzi kadhaa kuhusu polisi, wakati wa hotuba aliyoitoa katika shule ya kitaifa ya polisi huko Roubaix (kaskazini mwa Ufaransa). Hotuba hii ilifunga "vikao kuhusu usalama", mashauriano haya makubwa yaliyoanzishwa miezi 7 iliyopita.

Polisi watakuwa na "kituo cha mafunzo" juu ya kudumisha utulivu, ametangaza rais Macron wakati wa hotuba yake huko Roubaix.
Polisi watakuwa na "kituo cha mafunzo" juu ya kudumisha utulivu, ametangaza rais Macron wakati wa hotuba yake huko Roubaix. AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Emmanuel Macron anasema anataka "askari wawajibike kwa kazi yao", kwa maneno mengine, uwepo wa polisi katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuimarisha usalama zaidi. Hii inamaanisha, kulingana na rais wa Ufaransa, kuongezeka mara mbili katika kipindi cha miaka 10 ya uwepo wa maafisa wa polisi na askari wa jeshi kwenye maeneo ya umma.

"Lazima tuwaondoe maafisa wa  polisi katika majukumu ya kiutawala kwa kuendeleza na kuimarisha majukumu yao," almesema rais wa Ufaransa. Kuna haja pia ya kutathmini wakati wa kazi ili kuimarisha uwezo wa vitengo vilivyotumwa katika maeneo ya umma. "

Rais amesema alisikia ombi la wengi. Kwa hivyo ametangaza kuunda kikosi cha ziada cha maafisa wa polisi, kitaundwa na maafisa 30,000. Kikosi cha jeshi la polisi kiliyopo  kitaongezwa maafisa 20,000 wa ziada.

Katika ngazi ya kisiasa, rais Macron ametangaza kuwa sheria juu ya programu na usalama wa mwongozo itawasilishwa mapema 2022.

Emmanuel Macron amebaini kwamba jumla ya euro milioni 500 zitatolewa kwa utekelezaji wa mfumo wa usalama kuanzia mwaka 2022.

Kwa jumla, bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani itaongezeka kwa euro bilioni 1.5 mnamo 2022, ametangaza rais wa Ufaransa, akiwasilisha hitimisho la mashauriano haya makubwa juu ya usalama. Euro milioni 500 ni nyongeza ikilinganishwa na ongezeko la milioni 900 lililotangazwa na Waziri Mkuu Jean Castex mwishoni mwa mwezi Julai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.