Pata taarifa kuu
POLAND-HAKI

Poland yaona hatua za Mahakama ya EU ni kinyume na Katiba yake

Hatua za muda zilizowekwa na Mahakama ya Juu zaidi ya haki ya Umoja wa Ulaya dhidi ya mfumo wa mahakama ya Poland ni kinyume na katiba ya nchi hiyo, Mahakama ya Katiba ya Poland imesema Jumatano wiki hii, ikisababisha kuongezeka kwa uhasama wa kisiasa kati ya Warsaw na Brussels.

Katika kesi zilizozinduliwa mwaka jana na Brussels dhidi ya Poland, Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya iliomba Warsaw kusimamisha jopo lililoundwa ili kuwachukulia vikwazo majaji.
Katika kesi zilizozinduliwa mwaka jana na Brussels dhidi ya Poland, Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya iliomba Warsaw kusimamisha jopo lililoundwa ili kuwachukulia vikwazo majaji. REUTERS - Ints Kalnins
Matangazo ya kibiashara

Poland kwa muda mrefu imekuwa ikipingana na Umoja wa Ulaya (EU) juu ya kurekebisha mfumo wake wa mahakama, ambao chama tawala, Sheria na Haki (PiS) kinaeleza kuwa ni muhimu kuzifanya mahakama za nchi hiyo kuwa na ufanisi zaidi na kuondoa mabaki ya enzi ya ukomunisti.

Mbele ya wapinzani wa mageuzi hayo, hii ni njia ya Warsaw kuminya uhuru wa mahakama.

Katika kesi zilizozinduliwa mwaka jana na Brussels dhidi ya Poland, Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya mwaka jana iliomba Warsaw kusimamisha jopo lililoundwa ili kuwachukulia vikwazo majaji.

Ombi hili ni kinyume na Katiba ya Poland, imebaini Mahakama ya Katiba.

Brussels hapo awali ilitoa wito kwa Warsaw kutotilia shaka sheria ya Ulaya, ikielezea wasiwasi kwamba inapinga kanuni kuu za Umoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.