Pata taarifa kuu
UFARANSA

Julai 14: Ufaransa yaadhimisha Sikukuu ya Bastille Rais wa Ufaransa

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa kuongoza wananchi wa taifa hilo kuadhimisha siku ya Bastille (Bastille Day), kukumbuka mapinduzi yaliyotokea nchini humo mwaka 1789 na kumaliza uongozi wa Kifalme.

Kwa karibu masaa mawili, wanajeshi 4,400, wanaume kwa wanawake  watatumia barabara maarufu ya Paris kufanya maonesho yao. Gwaride hilo pia ilitahusisha farasi, ndege za kivita na helikopta.
Kwa karibu masaa mawili, wanajeshi 4,400, wanaume kwa wanawake watatumia barabara maarufu ya Paris kufanya maonesho yao. Gwaride hilo pia ilitahusisha farasi, ndege za kivita na helikopta. AP - Lewis Joly
Matangazo ya kibiashara

Kila Julai 14, Paris inaadhimisha Sikukuu ya Bastille (inayoitwa La Fête de la Bastille au la La Fête Nationale kwa Kifaransa), ambayo inaonyesha kushambuliwa kwa gereza la Bastille mnamo 1789 na tukio la kwanza kuu la Mapinduzi ya Kifaransa ya 1789.

Kinyume na ilivyokuwa miaka iliyopita, watu 10,000 wanatarajiwa kushuhudia maadhimisho ya siku hii jijini Paris, kutokana na tahadhari ya janga la COVID-19, huku guaride la jeshi likitarajiwa kushuhudiwa.

Kwa karibu masaa mawili, wanajeshi 4,400, wanaume kwa wanawake  watatumia barabara maarufu ya Paris kufanya maonesho yao. Gwaride hilo pia ilitahusisha farasi, ndege za kivita na helikopta

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.