Pata taarifa kuu
UFARANSA

Ufaransa yatangaza masharti zaidi ya kudhibiti aina mpya ya kirusi cha Corona

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza masharti zaidi ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona, wakati huu aina mpya ya maambukizi inayotwa Delta inapoendelea kusambaa kwa kasi.

Rais Emmanuel Macron wakati wa hotuba yake kwa Wafaransa, Julai 12, 2021
Rais Emmanuel Macron wakati wa hotuba yake kwa Wafaransa, Julai 12, 2021 © Élysée
Matangazo ya kibiashara

Macron amesema utoaji wa chanjo utakuwa lazima kwa wahudumu wa afya, huku akitoa wito kwa raia wa nchi hiyo kwenda kupata chanjo, wakati huu serikali inapoanza kuwahamasisha watu nchini humo

Hii ni hotua ya 8 ya televisheni ya Rais Macron tangu kuzuka kwa mgogoro huu wa kiafya nchini Ufaransa. Julai 12, Emmanuel Macron alitangaza hatua mpya za kuzuia mlipuko wa nne wa aina ya kirusi kipya cha Delta kinachoambukia haraka.

Emmanuel Macron ametangaza chanjo ya lazima kwa wauguzi na wafanyakazi wasio wauguzi katika hospitali mbalimbali, kliniki, nyumba za wazee, na pia kwa wataalamu na watu wanaojitolea kwa kuhudumia wazee.

Wahusika "wamepewa muda hadi Septemba 15 kuwa wamefanyiwa chanjo" na baada ya tarehe hii, kutafanyika "ukaguzi na vikwazo", ameongeza katika hotuba yake kwenye runinga.

Emmanuel Macron pia alitangaza kwamba "kampeni za chanjo" dhidi ya Covid-19 zitafanyika "tangu mwanzoni wa mwaka wa shule" kwa wanafunzi wa shule za upili na vyuo vikuu.

Hali ya dharura ya afya Martinique na Réunion

Hali ya dharura ya kiafya itatangazwa Jumanne, Julai 13 huko Martinique na Kisiwa cha Reunion na sheria ya kutotoka nje itatekelezwa katika maeneo hayo kwa sababu ya kuongezeka kwa idadi ya kesi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.