Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Euro: Johnson alaani "matusi ya kibaguzi" dhidi ya wachezaji wa Uingereza

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amelaani"matusi ya kibaguzi" yaliyolenga wachezaji wa wa tim ya taifa ya Uingereza baada ya kushindwa dhidi ya Italia katika fainali ya Euro Jumapili Julai 11 huko Wembley.

Mchezaji wa England, Luke Shaw na Philips wakimfariji Bukayo Saka, baada ya kukosa penati dhidi ya Italia.
Mchezaji wa England, Luke Shaw na Philips wakimfariji Bukayo Saka, baada ya kukosa penati dhidi ya Italia. FACUNDO ARRIZABALAGA POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Timu hii ya Uingereza inastahili kuchukuliwa kama mashujaa, na hapana kama (waathiriwa) wa matusi ya kibaguzi kwenye mitandao ya kijamii. Wale wanaohusika na dhuluma hizi za kutisha wanapaswa kujionea haya, ”kiongozi huyo wa kihafidhina ameisema kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Nchini Italia wananchi wameendelea kusherehekea ushindi wao usiku kucha jijini Rome, baada timu yao inayofahamika kama the  Azzuris kutawazwa mabingwa wa soka barani Ulaya, mashindano makubwa yanayotazamwa duniani.

Hili ni taji la pili la Italia, baada ya kushinda mara ya kwanza mwaka 1968.

Hata hivyo, ni masikitiko makubwa kwa Uingereza ambayo ilikuwa inasaka taji lake la kwanza. Mashabiki wa Uingereza waliamini kuwa kombe hilo lingebaki London.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.