Pata taarifa kuu
EU-URUSI

Ujerumani na Ufaransa zapendekeza kufanyika mkutano wa Umoja wa ulaya, na Urusi

Wiki moja baada ya kufanyika kwa mkutano kati ya rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin huko Geneva, Usuisi,  Ufaransa na Ujerumani zimependekeza kuandaa mkutano kama huo katika Jumuiya ya Ulaya.

Emmanuel Macron, Angela Merkel na Vladimir Poutine wakijadiliana katika Ikulu ya champs Elysee huko Paris Desemba 9, 2019.
Emmanuel Macron, Angela Merkel na Vladimir Poutine wakijadiliana katika Ikulu ya champs Elysee huko Paris Desemba 9, 2019. © AP - Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Pendekezo hili linakuja saa kadhaa baada ya tume ya umoja huo wa ulaya inayojihusisha na masuala ya kisiasa kukutana alhamisi ya juni 24 mwaka huu, ambapo wakuu wa nchi na serikali za Jumuiya ya Ulaya wamejadili suala la siasa za Urusi  na Marekani, lakini pia uhusiano wa kidiplomasia kati ya Urusi na mataifa ya Ulaya.

Mwandishi wa RFI aliyeko jijini Brussels, Ubelgiji Pierre Benazet anasema utawala wa Berlin na Paris hapo jana waliwasilisha pendekezo la kuzitaka nchi hizo kutafakari wazo la mkutano unaowezekana na Putin baada ya kukaa na Rais wa Marekani  Joe Biden huko Geneva wiki iliyopita.

Pendekezo hili la Berlin na Paris kuhusu kuandaliwa mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa umoja wa ulaya na Urusi limekubaliwa na ofisi ya mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell

Ujerumani na Ufaransa zimekuwa zikiishutumu Urusi kwa kuwakandamiza wapinzani, ikiwa ni pamoja na kushikiliwa kwa mwanasiasa wa upinzani Alexeï Navalny lakini pia kuchochea siasa za Ukraini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.