Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Uingereza: Boris Johnson alengwa na uchunguzi juu ya ukarabati wa nyumba yake

Tume ya Uchaguzi ya Uingereza imesema leo Jumatano kuwa imefungua uchunguzi rasmi juu ya mipango ya ufadhili wa ukarabati wa ghorofa ya Boris Johnson huko Downing Street, baada ya mshirika wake wa zamani kupendekeza kwamba aliweza kupata ufadhili haramu.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Jonhson amekuwa akikabiliwa kwa siku kadhaa na shinikizo kubwa juu ya la kupata ufadhili haramu.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Jonhson amekuwa akikabiliwa kwa siku kadhaa na shinikizo kubwa juu ya la kupata ufadhili haramu. REUTERS/Virginia Mayo/Pool
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na shirika la habari la REUTERS, Waziri Mkuu wa Uingereza amekuwa akikabiliwa na shinikizo kubwa juu ya suala hili kwa siku kadhaa.

"Sasa tuna uhakika kuwa kuna sababu nzuri za kushuku kwamba kosa moja au zaidi yametendeka," imesema tume ya uchaguzi katika taarifa.

"Kwa hivyo tutaendelea na kazi hii na uchunguzi rasmi" kubaini ikiwa shughuli zinazohusu kazi hii ziko chini ya udhibiti wa ufadhili wa maisha ya kisiasa ambapo tume hii huru inawajibika na ikiwa ufadhili wa shughuli hizi umetangazwa kama inavyotakiwa.

Tume ya uchaguzi inasisitiza kuwa haitatoa maoni yoyote ya ziada kabla ya kumalizika kwa uchunguzi

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.