Pata taarifa kuu
UJERUMANI

Coronavirus: Idadi ya vifo nchini Ujerumani yazidi 80,000

Ujerumani imerekodi visa vipya 11,437 vilivyothibitishwa vya vya maambukizi ya virusi vya Corona, kulingana na takwimu zilizotolewa lzo Jumatatu na Taasisi inayokabiliana na Magonjwa ya Kuambukiza ya Robert Koch (RKI), na kufikisha jumla ya maambukizi 3,153,699 tangu kuzuka kwa ugonjwa huo nchini humo.

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na viongozi wengine wa serikali wanahudhuria sherehe ya kumbukumbu ya wahanga wa ugonjwa wa Corona (COVID-19), huko Berlin, Ujerumani Aprili 18, 2021
Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na viongozi wengine wa serikali wanahudhuria sherehe ya kumbukumbu ya wahanga wa ugonjwa wa Corona (COVID-19), huko Berlin, Ujerumani Aprili 18, 2021 via REUTERS - JESCO DENZEL
Matangazo ya kibiashara

RKI pia imeripoti vifo vipya 92 vilivyotokana na COVID-19, kwa na kufikisha idadi ya vifo 80,006.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la habari la Ufaransa, AFP zaidi ya vifo 12,000 duniani kote viliripotiwa kila siku katika muda wa wiki moja iliyopita na kupindukia vifo milioni tatu kufikia Jumamosi.

Janga hilo halionyesha dalili ya kupunguza makali yake, huku watu 829,596 wakiambukizwa virusi vya corona siku ya Ijumaa pekee, idadi hiyo ikiwa ya juu zaidi kwa watu kuambukizwa kwa siku moja.

Siku ya Jumapili Ujerumani ilifanya ibada maalum ya kitaifa kuwakumbuka takriban watu 80,000 waliokufa kwa ugonjwa wa COVID-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.