Italia yafungwa kipindi chote cha sikukuu ya Pasaka
Nchi ya Italia imefungwa kwa siku tatu, katika kipindi hiki cha pasaka ili kupambana na ongezeko la maambukizi ya Covid 19.
Imechapishwa:
Hatua hii imekuja baada ya nchi hiyo kuanza kuripoti visa vya maambukizi 20,000 kila siku, katika siku za hivi karibuni.
Maeneo yote ya nchi hiyo sasa yapo katika hali ya hatari kuafutia ongezeko hilo.
Watu wamezuiwa kutembea, lakini wameruhusiwa kushiriki chakula cha pamoja nyumbani siku ya Pasaka.
Makanisa hayajafungwa lakini waumini, wameshauriwa kuhudhuria ibada katika maeneo wanayoishi.
Kwa mwaka wa pili, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis atalazimika kutoa mahubiri yake siku ya Jumapili kwenye uwanja mtupuu wa Mtakatifu Peter, mjini Vatican kufuatia janga la Covid 19.
Tangu kuzuka kwa maambukizi ya corona, watu zaidi ya Laki Moja na Elfu 10 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya Milioni 3.6 wameambukizwa.