Pata taarifa kuu
UHOLANZI- AFYA

Uholanzi Mahakama kutoa uamuzi kuhusu sheria ya kutotoka nje Ijumaa ijayo

Mahakama ya Uholanzi itatoa uamuzi Ijumaa ijayo baada ya wanaharakati mbalimbali kukata rufaa kuhusu uhalali wa sheria ya kutotoka nje iliyowekwa na serikali ya Uholanzi ili kupunguza maambukizi ya virusi vya Corona inayosababisha ugonjwa wa COVID-19, jaji wa mahakama ya rufaa amesema.

Waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte akitangaza makataa ya kutotoka nje ili kupambana na Covid-19   october 13 2020.
Waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte akitangaza makataa ya kutotoka nje ili kupambana na Covid-19 october 13 2020. AP Photo/Olivier Matthys, Pool
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne mahakama ya mwanzo ya wilaya ya Hague iliamua kwamba hatua hii haikuwa halali na inapaswa kubatilishwa. Serikali ilikata rufaa mara moja, hali ambayo ilisitisha uamuzi huo.

Baraza la Seneti linajadili muswada uliopitishwa haraka na serikali ya Mark Rutte ambao ungeipa serikali mamlaka ya kuendelea kushikilia sheria hiyo ya kutotoka nje.

Wapinzani wanasema sheria hii ya kutotoka nje, ikiwa ni sheria ya kwanza nchini Uholanzi tangu vita vya pili vya dunia, ni kizuizi kisichohitajika kwa uhuru.

Sheria hiyo iliyowekwa mnamo Januari 23 na kuongezwa muda hadi Machi 3, inapiga marufu watu kutotoka nje kati ya saa tatau usiku na saa kumi na nusu Alfajiri, isipokuwa kwa kwa yule aliyepewa kibali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.