Pata taarifa kuu
UHOLANZI

Mahakama kutoa uamuzi kuhusu sheria ya kutotoka nje Ijumaa ijayo

Mahakama ya Uholanzi itatoa uamuzi Ijumaa ijayo baada ya wanaharakati mbalimbali kukata rufaa kuhusu uhalali wa sheria ya kutotoka nje iliyowekwa na serikali ya Uholanzi ili kupunguza maambukizi ya vurusi vya Coronainayosababisha ugonjwa wa COVID-19, jaji wa Mahakama ya Rufaa amesema.

Watalaam wa afya wanaopambana na janga la Corona
Watalaam wa afya wanaopambana na janga la Corona REUTERS/Lucy Nicholson
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne mahakama ya mwanzo ya wilaya ya Hague iliamua kwamba hatua hii haikuwa halali na inapaswa kubatilishwa. Serikali ilikata rufaa mara moja, hali ambayo ilisitisha uamuzi huo.

Baraza laS eneti linajadili muswada uliopitishwa haraka na serikali ya Mark Rutte ambao ungeipa serikali mamlaka ya kuendelea kushikilia sheria hiyo ya kutotoka nje.

Wapinzani wanasema sheria hii ya kutotoka nje, ikiwa ni sheria ya kwanza nchini Uholanzi tangu vita vya pili vya dunia, ni kizuizi kisichohitajika kwa uhuru.

Sheria hiyo iliyowekwa mnamo Januari 23 na kuongezwa muda hadi Machi 3, inapiga marufu watu kutotoka nje kati ya saa tatau usiku na saa kumi na nusu Alfajiri, isipokuwa kwa kwa yule aliyepewa kibali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.