Pata taarifa kuu
UHOLANZI

Uholanzi yaendelea kukumbwa na vurugu kufuatia sheria ya kutotoka nje

Kama siku iliyopita, ghasia zilizuka Jumatatu hii usiku katika miji kadhaa nchini Uholanzi. Vurugu zilianza baada ya amri ya kutotoka nje iliyotangazwa mwishoni mwa juma lililopita  kwa kujaribu kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona na aina mpya ya kirusi cha Corona nchini humo. 

Hali ilivyo katika uwanja wa ndege wa Serbia
Hali ilivyo katika uwanja wa ndege wa Serbia REUTERS/Marko Djurica
Matangazo ya kibiashara

Rotterdam, Amsterdam, The Hague ... Karibu miji kumi ya Uholanzi ilikumbwa na ghasia hizo Jumatatu usiku.  Fataki na mawe vilirushwa dhidi ya polisi.

Katika mji wa Amsterdam, wafanya ghasia walijaribu kuchoma moto gari la polisi, lakini maafisa wa polisi waliingilia kati na kuwatimua.

Uporaji wa maduka pia umeripotiwa katika maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na miji mikubwa nchini humo.

Sheria ya kutotoka nje imeendelea kupingwa na sehemu kubwa ya raia wa Uholanzi

Vurugu hizo zilianza kuibuka Jumapili, siku ya pili ya sheria ya kutotoka nje iliyotangazwa na serikali kwa matumaini ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona.

Baada ya Waziri Mkuu kuthibitisha kesi ya kwanza ya maambukizi ya aina mpya ya kirusi cha Corona kiliyozuka hivi karibuni, serikali ilitangaza sheria ya kutotoka nje, lakini sehemu kubwa ya raia wa nchi hiyo wamepinga sheria hiyo wakibaini kwamba sheria hiyo inakuja kuvunja uhuru wa umma.

Marufuku hii ya kutotoka nje baada ya saa tatu usiku ni ya kwanza kutolewa nchini Uholanzi tangu kumalizika kwa Vita vya pili vya Dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.