Pata taarifa kuu
UJERUMANI-UFARANSA-UTURUKI-USHIRIKIANO

Berlin yashikamana na Paris na kushutumu mashambulizi ya Uturuki

Mashambulizi ya rais wa Uturuki Erdogan akihoji "afya ya akili" ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na wito wa Ankara kutaka kususiwa kwa bidhaa za Ufaransa kupinga hatua zilizochukuliwa na Paris kupambana na Uislam wenye itikadi kali, washirika wa Ufaransa wameanza kuchukua hatua.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Maas (hapa ilikuwa Berlin Oktoba 26, 2020) alielezea mshikamano wa nchi yake na Ufaransa, hasa katika vita vyake dhidi ya Uislamu wenye itikadi kali.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Maas (hapa ilikuwa Berlin Oktoba 26, 2020) alielezea mshikamano wa nchi yake na Ufaransa, hasa katika vita vyake dhidi ya Uislamu wenye itikadi kali. Michael Sohn/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa ilichukuwa hata hiyo baada ya mauaji ya mwalimu Samuel Paty, aliyejinjwa na muislamu mwenye itikadi kali za kidini.

Rais Macron alisema Ufaransa haitoacha kuchora vibonzo, kutokana na kuchinjwa kwa mwalimu Samuel Paty aliyewaonesha wanafunzi wake kibonzo cha Mtume Muhammad mapema mwezi huu, katika kitongoji kimoja cha Paris katika somo kuhusu uhuru wa kujieleza.

Siku ya Ijumaa vibonzo vya Mtume Muhammad vilichapishwa kwenye majengo ya serikali nchini Ufaransa, hatua iliyokasirisha nchi za Kiarabu.

Ujerumani imesema inashikamana na Ufaransa na haikubakiani na mashalmbulizi ya Uturuki dhidi ya Ufaransa na rais wake.

Wakati huo huo baadhi ya nchi za Kiislam zimetoa wito wa kususia bidhaa za Ufaransa ikiwa ni katika kuijibu hatua ya rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron kuunga mkono kitendo cha kuchorwa kibonzo cha Mtume Muhammad.

Hatua ya wito wa kususia bidhaa zinazotengezwa nchini Ufaransa unaendelea kushuhudiwa kwenye mitandao ya kijamii, huku wananchi wa Misri wakisambaza orodha ya bidhaa za kutoka Ufaransa wanazotaka zisusiwe.

Huko nchini Kuwait, mashirika zaidi ya Hamsini ya kibiashara yamesema yameondoa bidhaa zote za Ufaransa katika maduka yake.

Hata hivyo, serikali ya Ufaransa imekosoa wito wa kususiwa kwa bidhaa zake, na kutaka ikomeshwe na kusema hizo ni kauli za Waislmau wachche wenye msimamo mkali.

Katika hatua nyingine, Wizara ya mambo ya nje ya Pakistan imemuita balozi wa Ufaransa nchini humo kulalamika kuhusu kitendo cha Rais Macron kuunga mkono kuchapishwa vibonzo vya Mtume Muhammad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.