Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya vifo nchini Ujerumani yaongezeka hadi zaidi ya 9,400

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 275,927, baada ya visa vipya 1,769 kuthibitishwa katika muda wa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Jumatano na Kituo cha kuzuia na Kudhibiti magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Ujerumani inaendelea kurekodi visa zaidi vya maambukizi.
Ujerumani inaendelea kurekodi visa zaidi vya maambukizi. Ina FASSBENDER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na RKI, vifo vipya kumi na tatu vimeripotiwa, na kufanya jumla ya vifo kufikia 9,409 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Hayo yanajiri wakati idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Marekani kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona, sasa imeongezeka na kufikia zaidi ya Laki Mbili, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

Pamoja na vifo hivyo, watu wengine Milioni Sita na Laki Nane, wameambukizwa virusi hivyo na kuifanya Marekani kuwa nchi yenye maambukizi makubwa duniani.

Utafiti unaonesha kuwa idadi ya vifo imeongezeka baada ya maambukizi hayo kuongezeka maradufu katika siku za hivi karibuni katika maeneo ya Dakota Kaskazini na Utah.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.